Posts

Showing posts from August 4, 2013

CLOUDS MEDIA GROUP YAPATA IFTAR YA PAMOJA NA WADAU WAKE

Image
 Kampuni ya Clouds Media Group mwishoni mwa wiki iliandaa Ftari ya pamoja kwa wafanyakazi wake na baadhi ya wadau mbalimbali,maeneo ya Sinza-jijini Dar Salaam.Pichani kushoto ni  Mkurugenzi wa vipindi na utafiti,Ruge Mutahaba pamoja na Meneja Vipi wa Clouds FM Sebastian Maganga wakiongoza wageni waalikwa mbalimbali kupata ftari.Pichani chini ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na wadau wengine waalikwa wakijipakulia ftari safi kabisa. Sehemu ya Wadau wakiendelea kupata ftari. Picha na Jiachie Blog.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUTURISHA CHAKECHAKE PEMBA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki katika swala ya Magharibi na baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, wakati wa hafla ya futari ya pamoja aliyoiandaa katika Makazi yake Ikulu ndogo Mjini Pemba jana Agosti 7, 2013. Picha na OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki futari ya pamoja na baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, aliyoiandaa katika Makazi yake Ikulu ndogo Mjini Pemba jana Agosti 7, 2013. Picha na OMR   Baadhi ya wananchi wa Pemba walioshiriki katika futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jana. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wageni wake baada ya kushiriki nao futari ya pamoja aliyoiandaa katika makazi yake Ikulu ndogo mjini Pemba, jana Agosti 7, 2013. Picha na OMR

RAIS DKT. KIKWETE NA MAMA SALMA WAMJULIA HALI MH.JOHN MOMOSE CHEYO

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali mwenyekiti wa UDP Mh.John Momose Cheyo aliyelazwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.Katikati ya Rais na Mama Salma ni Mjukuu wa  Mheshimiwa Cheyo anayejulikana kama Gabriel Cheyo. (Picha Freddy Maro)

WAZIRI MKUU MHE. PINDA AZUNGUMZA NA WATANZANIA LONDON

Image
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakisalimiana na baadhi ya watumishi  wa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza  uliopo London baada ya kuwawsili kwenye ubalozi huo kuzungumza na watanzania waishio Uingereza Agosti 6, 2013. (Picha na Ofisi ya Wazire Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakisalimiana na Watoto Tanzania nchini Uingereza uliopo London  kuzungumza na watanzania waishio Uingereza Agosti 6,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  baadhi ya Watanzania waishio Uingereza  kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo London Agosti 6,2013. Kushoto ni Mkewe Tunu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu ) Baadhi ya Watanzania waishio London wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza  nao kwenye ubalozi wa Tanzania nchini humo uliopo Londoni Agosti 6, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakiwa katika picha ya pamoja na badhi ya Uingereza...

BALOZI WA KENYA NCHINI AMUAGA RAIS DK.SHEIN

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe,Mutinda Mutiso,alipofika Ilkulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais, baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na  Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe,Mutinda Mutiso,alipofika Ilkulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,akiwa amemaliza  muda wake wa kazi Nchini.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifuatana na Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mhe,Mutinda Mutiso,alipofika Ilkulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]