SAFARI LAGER YASHEREHEKEA USHINDI WAKE NA WAHESHIMIWA WABUNGE MJINI DODOMA
Mgeni Rasmi kwenye hafla ya Kupongeza Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Anne Makinga (katikati) akiwa amenyanua juu moja ya vikombe vya ushindi huo ikiwa ni ishara ya kuzindua ziara Bia hiyo katika mikoa mbali mbali hapa nchini ili kuwaonyesha Watanzania ushindi huo. Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinga akitoa hotuba yake fupi kwa waheshimiwa Wabunge na Wageni waalikwa waliokuwepo kwenye hafla hiyo iliyofanyika usiku huu kwenye viwanja vya Bunge,Mjini Dodoma. Mkurugenzi wa Miradi Maalum wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Phocas Laswai akitoa hotuba yake mbele ya Mgeni Rasmi,Viongozi mbali mbali pamoja na wageni waalikwa waliohudhulia hafla hiyo iliyofanyika usiku huu kwenye Viwanja vya Bunge,Mjini Dodoma. Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo akiutambulisha Ujumbe wa TBL ulioambatana nae kwenye ziara hiyo. Mpishi Mkuu wa Bia za TBL,Gaudence Mkolwe (kulia) akitoa ufafanuzi...