Posts

Showing posts from November 17, 2013

Rais Jakaya Kikwete Ahitimisha Ziara Yake Nchini Poland

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Fatma Fereji wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Nchi katika Makamu wa Rais Dkt Tereiya Huvisa wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Katibu Mkuu  katika Ofisi ya Makamu wa  Rais  Mhe Sazi Salula  wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Po...

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA FINLAND NCHINI

Image
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akimkaribisha Ofisi kwake Balozi wa Finland hapa nchini Mhe. Sinikka Antila alipofika kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Tanzania na Finland zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu katika masuala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na utawala bora. Mhe. Dkt. Maalim akimweleza jambo Mhe. Antila wakati wa mazungumzo yao. Mhe. Antila naye akifafanua jambo kwa Mhe. Dkt. Maalim wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Bibi Victoria Mwakasege (kulia mwenye nguo ya njano), Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Ulaya na Amerika akifuatiwa na Bi. Upendo Mwasha, Afisa Mambo ya Nje. Kushoto ni Bw.Jussi Nummelin, Afisa katika Ubalozi wa Finland hapa nchini.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYIWA MAOMBI OFISINI KWAKE LEO

Image
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa amepiga magoti kama ishara ya unyenyekevu huku akiwa amewekewa mikono na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali waliokuwa wakimwombea ofisini kwake. Baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali wakisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kabla ya kuanza kwa kikao chao. Viongozi hao walifika kwa ajili ya kumpongeza Waziri Muhongo kwa kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kumfanyia maombi maalumu. Viongozi kutoka madhehebu mbalimbali wakiendelea kubadilishana mawazo mara baada ya kumaliza kikao chao na Waziri. Aliyesimama ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo. Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiagana na baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa kikao. Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa sita kutoka kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava ( wa pili ...

MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL, AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA AFRO – ARAB NCHINI KUWAIT

Image
Makamu wa Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal ameiwakilisha Tanzania katika mkutano wa mashirikiano baina ya nchi za Afrika na zile za Kiarabu, mkutano wa siku mbili unaofanyika katika nchini Kuwait.  Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika, wakati wakiwasili kwenye ukumbi wa Mkutano wa Tatu wa nchi za Kiarabu 'Afro Arab', uliofanyika nchini Kuwait, leo Mkutano huo unaohudhuriwa na viongozi wa nchi zaidi ya 70 unalenga kuimarisha ushirikiano wa Afrika na nchi za Kiarabu na unapitia makubaliano ya mkutano wa Sirte, Libya uliofanyika mwaka 2011. Mkutano huu unafanyika kukiwa na mabadiliko kadhaa ya kiasiasa, kiuchumi na kimkakati baina ya nchi za kanda hizi mbili huku taswira ya kukua kwa ushikiano huu zikionekana bayana kuwa muhimu zaidi sasa kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Hii inatokana na nchi za kanda hizi mbili, kukabiliwa na changamoto nyingi zina...

AFANDE SELE AJIUNGA CHADEMA MOROGORO

Image
Mwanamziki mashuhuri Tanzania, anayejulikana kama Afande Sele Amejiunga na M4C, kwa kuingia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. Mji wa morogoro ulirindima vifijo wakati Afande akizunguka na Msafara wa Piki Piki kuwaaga rasmi wale wasio na misimamo thabiti Kisiasa, kama inavyoonekana katika picha. kwa upande mwingine wapenzi wa CCM walionekana kuwa nahofu na uchungu, na walihisi sasa mambo yanazidi kuwa magumu sana kwao. Kata ya mafiga wa upande wake ilionekana kutekwa kabisa na CHADEMA, huku katika mkutano wa Ndani Afande Sele alichaguliwa kushika nafasi ya Uenyekiti wa kata hiyo, katika kipindi hiki cha kushusha chama kwa wananchi (Program ya Chadema ni msingi), ambayo imekuwa mwiba mkali kwa CCM. Mwanamziki mashuhuri Tanzania, anayejulikana kama Afande Sele Amejiunga na M4C, kwa kuingia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. Mji wa morogoro ulirindima vifijo wakati Afande akizunguka na Msafara wa Piki Piki kuwaaga rasmi wale wasio na misimamo thabiti Kisiasa, kama inavyoonekana kati...

WAZIRI MKUU MHE. PINDA AFUNGUA MKUTANO WA MAJAJI WA ARFIKA NA KUHUDHURIA MAZISHI YA DR. MVUNGI

Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana  na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande (kuhoto) na Rais wa Mahakama ya afrika Jaji  Sophia Kuffo kabla ya  kufungua mkutano wa majaji wa Afrika kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Novemba 18, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Askofu wa Jimbo, Geita Dmiano  Dallu akifukiza ubani mwili wa Dr. Edmund Mvungi katika ibada ya mazishi iliyofanyika  kijijini kwa marehemu, Chanjale wilayani Mwanga Novemba 18, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka shada la maua katika jeneza la marehemu Dr. Edmund Mvungi kabla ya azishi yaliyofanyika kijijini  kwa marehemu Chanjale  wilayani Mwanga Novemba 18, 2013. (Picha na Ofisi ya `Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Dr.Edmund Mvungi katika ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini kwa marehemu Chanjale wilayani Mwanga Novemba 18, 2013. (Picha  na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA WANACCM TUMBE

Image
Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar,Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM Tawi la Tumbe,wilaya ya Wete Pemba,akiwa katika ziara maalum, [ Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Wananchi na Wanachama wa CCM Jimbo la Tumbe wakimsikiliza Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar,Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza katika mkutano wa chama katika kijiji cha Tumbe,alipokuwa katika ziara maalum katika Wilaya ya Wete Pemba leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar,Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati)akisikiliza Risala ya wanachama CCM Tawi la Tumbe  iliyosomwa na Time Juma,

ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU SONGEA

Image
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu vya SAUT, St.Joseph na Chuo cha Ualimu Matogoro kwenye ukumbi wa Songea Club.  Wanafunzi wapatao 650 wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ukumbi wa Songea Club.  Mkuu wa Wilaya ya Songea mjini Ndugu Joseph Joseph Mkirikiti(wa kushoto) akiwa pamoja na wadau wa elimu wa Wilaya ya Songea wakimsikiliza Karibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo Songea .  Katibu wa Mkoa wa Vyuo vya Elimu ya Juu Ndugu Christopher Ngubiagai akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu vya mjini Songea wakati wa kikao cha wanafunzi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Klabu ya Songea Baadhi ya wanafunzi wakisikiliza kwa makini masuala mbalimbali yaliyokuwa yanajadiliwa kwenye kikao kilichowahisusha wanafunzi wa v...