NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA FINLAND NCHINI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akimkaribisha Ofisi kwake Balozi wa Finland hapa nchini Mhe. Sinikka Antila alipofika kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Tanzania na Finland zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu katika masuala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na utawala bora.
Mhe. Dkt. Maalim akimweleza jambo Mhe. Antila wakati wa mazungumzo yao.
Mhe. Antila naye akifafanua jambo kwa Mhe. Dkt. Maalim wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Bibi Victoria Mwakasege (kulia mwenye nguo ya njano), Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Ulaya na Amerika akifuatiwa na Bi. Upendo Mwasha, Afisa Mambo ya Nje. Kushoto ni Bw.Jussi Nummelin, Afisa katika Ubalozi wa Finland hapa nchini.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB