Posts

Showing posts from September 30, 2012

RAIS KIKWETE KATIKA ZIARA RASMI OTTAWA, CANADA

Image
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Mhe. John Baird baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Macdonald Cartier jijini Ottawa, Canada, kwa ziara rasmi ya siku mbili jijini  humo Jumatano Oktoba 4, 2012. ais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni huku akiangaliwa na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Mhe. John Baird baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Macdonald Cartier jijini Ottawa, Canada, kwa ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika viwanja vya jumba la Rideau Hall jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya  kuanza ziara rasmi ya siku mbili jijini  humo Jumatano Oktoba 4, 2012. Jumba hilo ndilo makazi  na ofisi rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada tangia mwaka 1867 ambapo pamoja na kuishi humo pia hapo ndipo hutumika kwa kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya vyema, pa kupokelea wageni mashuhuri wa nchi

TANZANIA KUZIDI KUIMARISHA MAHUSIANO NA INDIA – SPIKA MAKINDA

Image
Spika wa Bunge la India Mhe. Meira Kumar akimkaribisha mgeni wake, Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Anne Makinda kwenye chumba maalum kwa ajili ya mazunguzo kuhusu ushirikiano wan chi mbili hizi . Mhe. Makinda akisaini kitabu cha wageni mshuhuri huku akiongozwa na mwenyeji wake, Mhe. Kumar Mhe. Makinda akisaini kitabu cha wageni mshuhuri huku akiongozwa na mwenyeji wake, Mhe. Kumar Pokea zawadi kutoka Tanzania… ndivyo Spika Mkakinda anavyomwambia mwneji wake. Baada ya mkutano wa Saba wa Maspika wa Bunge wanawake kumalizika, viongozi hao kwa pamoja walikutana na waandishi wa habari na kuwaeleza yaliyojiri. Kwaheri na karibu Tanzania Ujumbe wa Tanzania na ule wa india kwa pamoja  Picha na Prosper Minja wa Bunge (kwa picha zaidi tembelea:  www.prince-minja.blogspot.com

Rick Ross atua Dar

Image

UJERUMANI YAIMWAGIA TANZANIA BILIONI 352

Image
Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa(kushoto) na Balozi wa Ujerumani nchini Kluas Peter Brandes (kulia) wakisaini mkataba wa msaada wa miaka mitatu juzi mjini Dar es salaam  ambapo Ujerumani itaipatia  Tanzania msaada wa Shilingi bilioni 352 . Msaada huo utasaidia kuboresha utawala bora katika serikali za mitaa, sekta ya afya , nishati , maliasili, maji, mfuko wa bajeti ya Serikali na kuboresha programu ya usimamizi wa fedha za umma. Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa(kushoto) na Balozi wa Ujerumani nchini Klaus Peter Brandes (kulia) wakibadilishana hati za makubaliano ya mkataba wa msaada wa miaka mitatu mjini Dar es salaam  ambapo Ujerumani itaipatia Tanzania msaada wa Shilingi bilioni 352 . Msaada huo utasaidia kuboresha utawala bora katika serikali za mitaa, sekta ya afya , nishati , maliasili, maji, mfuko wa bajeti ya Serikali na kuboresha programu ya usimamizi wa fedha za umma. Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa(kushoto) akisoma hotuba mara baada ya kusaini hati ya maku

ZIARA YA RAIS KIKWETE YAZAA MATUNDA APATA BILIONI 24.1 KWA AJILI YA AFYA

Image
Matajiri wawili wakubwa duniani jana, Jumanne, Oktoba 2, 2012, wameichangia Tanzania kiasi cha sh. bilioni 24.1 (sawa na dola za Marekani milioni 15.5) kwa ajili ya kuendeleza afya ya akinamama na kusaidia uzazi salama hasa katika maeneo ya vijijini. Matajiri hao, Mheshimiwa Michael Bloomberg ambaye ni Meya wa Jiji la New York, Marekani na Mama Helen Agerup wa Sweden, wametangaza mchango wao huo mkubwa kwa Tanzania kwenye mkutano maalum wa waandishi wa habari uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. Pamoja na matajiri hao kwenye mkutano huo wa waandishi wa habari walikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Ban Ki Moon. Kati ya fedha hizo, Meya Bloomberg wa Jiji la New York lenye wakazi milioni 8.4, anatoa kiasi cha dola za Marekani milioni nane kupitia Taasisi yake ya Bloomberg Philanthropies wakati Mama Agerup anatoa kiasi cha dola milioni 7.5 k

Dr Slaa kutikisa Arusha Jumamosi

Image
 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika jiji la Arusha siku ya Jumamosi tarehe 06.10.2012 kuanzia saa 8 mchana. Pamoja na mambo mengine Kiongozi huyo wa CDM pia atatumia mkutano huo kuzindua rasmi kampeni za udiwani katika kata ya daraja mbili,uzinduzi huo utafanyika katika viwanja vilivyopo mtaa wa NDARVOI. Tayari kuna hekaheka kubwa katika jiji la Arusha kuhusiana na mkutano huo ambapo mazungumzo ya watu mbalimbali yanazungumzia mkutano huo unaotarajiwa kuwa gumzo. Taarifa za awali zinasema mkutano huo pia utatumika kufuta nyayo za chama cha CUF ambacho kilisomba watu Dar-es-Salaam kwenda kuwahutubia Arusha ili kuepuka aibu ya kukosa watu.Pia inadaiwa wananchi wa Arusha wamedhamiria kuonyesha dunia uungaji mkono wao kwa chama cha CDM.

PICHA ZA MKUTANO WA CHADEMA KARATU

Image

Zimbabwe's President motorcade in 4th fatal crash

Image
Zimbabwe President Robert Mugabe in his official car. A police outrider in Mr Mugabe’s motorcade was burnt beyond recognition on Wednesday in the fourth fatal road accident involving the veteran ruler’s escort this year.  BBC A police outrider in Zimbabwe President Robert Mugabe’s motorcade was burnt beyond recognition on Wednesday in the fourth fatal road accident involving the veteran ruler’s escort this year. Police said the biker who was clearing traffic for the motorcade collided with a truck in Harare’s leafy suburb of Borrowdale where President Mugabe has his private residence in the morning. “It was a fatal accident and next of kin are yet to be informed, so we can’t give the name of the deceased,” assistant police spokesperson Charity Charamba said on Thursday. She said investigations were still underway to establish the cause of the accident. The driver of the truck Mr Cliff Moyo told local media that he was hit as he tried to negotiate a turn. “It wa

DK.SHEIN AFUNGA SEMINA YA VIONGOZI

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,DK.Ali Mohamed Shein,pia Mwenyekiti wa Semina ya Kuimarisha Uhusiano Baina ya  Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akibadilishana mawazo na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,mara baada ya kuifunga semina hiyo jana,katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort, Nje kidogo ya Mji wa Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Viongozi mbali mbali wakiwa wajumbe wa Semina ya Kuimarisha Uhusiano Baina ya  Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,wakitoka nje ya ukumbi wa mkutano baada ya kumaliza kwa mkutano huo jana,Zanzibar Beach Resort, Nje kidogo ya Mji wa Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

PRESIDENT KIKWETE MEETS WITH UN’S SECRETARY GENERAL

Image
H.E. Jakaya Mrisho Kikwete (left), President of the United Republic of Tanzania met with Mr. Ban Ki-moon, United Nations Secretary General for official talks at the United Nations Headquarters in New York, USA. President Kikwete (left) signing visitor’s book before UN’s Secretary General Ban Ki-moon. President Kikwete in discussion with UN’s Secretary General Ban Ki-moon during their meeting at the United Nations Headquarters in New York, USA. President Kikwete in a photo with Mr. Ban Ki-moon.(Photos by Mrs. Maura Mwingira of the Tanzania Mission to the United Nations).

PINDA AHUDHURIA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MANSOOR DAYA

Image
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwasha moja ya mtambo wa kutengeneza dawa wakati alipotembelea kiwanda  cha dawa za binadamu cha Mansoor Daya Chemicals  cha jijini Dar es salaam kilichotimiza miaka 50 Oktoba 2, 2012. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Mansoor Daya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Bwana Mansoor Daya (kulia kwake) na familia yake baada ya kutembelea  na kuzungumza  wafanyakazi na waalikwa  wa kiwanda cha dawa za binadamu cha Mansoor Daya Chemicals Limited cha jijijini Dar es salaam kilichotimiza miaka 50 Oktoba 2, 2012. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akikagua utengenezaji dawa za binadamu wakati alipotembelea kiwanda cha dawa za binadamu cha  Mansoor Chemicals Limited cha jijini Dar es salaam kilichotimiza miaka 50, Oktoba 2, 2012. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Mansoor Daya.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Rais Jakaya Kikwete Ziara ya Kikazi ya Marekani na Ziara Rasmi ya Kiserikali ya Canada akianzia mjini New York

Image
Rais Jakaya Kikwete  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaanza Ziara ya Kikazi ya Marekani na Ziara Rasmi ya Kiserikali ya Canada akianzia mjini New York, Marekani leo,Jumatatu, Oktoba Mosi, 2012. Rais Kikwete na ujumbe wake uliondoka nchini usiku wa jana, Jumapili, Septemba 30, 2012, na utawasili mjini New York, Marekani mchana wa leo tayari kwa ziara hiyo ya Marekani. Rais Kikwete atakuwa Marekani kwa siku mbili kabla ya kwenda Canada kwa ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili.  Katika ziara yake mjini New York, Marekani, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki Moon ofisini kwa Katibu Mkuu huyo kesho asubuhi Oktoba 2, 2012. Baada ya mazungumzo hayo, Rais Kikwete ataungana na Mheshimiwa Ban Ki Moon, Meya wa Jiji la New York na Mfadhili Mkubwa wa Misaada yaKibinadamu Duniani, Mheshimiwa Michael Bloomberg; Mama Helen Agerup ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mis

PICHA ZA SHILOLE NA AUNT EZEKIEL WALIVOFANYA BALAA KUBWA MTWARA

Image