WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYIWA MAOMBI OFISINI KWAKE LEO

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa amepiga magoti kama ishara ya unyenyekevu huku akiwa amewekewa mikono na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali waliokuwa wakimwombea ofisini kwake.
Baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali wakisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kabla ya kuanza kwa kikao chao. Viongozi hao walifika kwa ajili ya kumpongeza Waziri Muhongo kwa kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kumfanyia maombi maalumu.
Viongozi kutoka madhehebu mbalimbali wakiendelea kubadilishana mawazo mara baada ya kumaliza kikao chao na Waziri. Aliyesimama ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiagana na baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa kikao.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa sita kutoka kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava ( wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa kikao.
MICHUZI BLOG

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB