UJUMBE WA PONGEZI KUTOKA KWA RAIS WA TANZANIA KWA UHURU KENYATTA


“Mpendwa Rais Mteule na Kaka, ilikuwa ni furaha
kubwa kwangu kupokea taarifa ya ushindi wako wa
kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Niruhusu,
 kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Tanzania, na kwa
 hakika, kwa niaba yangu binafsi kukupogenza kwa dhati
ya moyo wangu kwa mafanikio haya makubwa ya
kuchaguliwa kwako.”

Ameongeza Rais Kikwete: “ Ushindi huu ni ushahidi na
ishara ya wazi kabisa ya imani na matumaini ambayo
wananchi wa Kenya waliyonayo katika uongozi wako. Huu ni
 utambuzi wa kazi yako maridadi na mchango wako mkubwa
 ambao umeutoa katika nafasi mbali mbali za uongozi katika
 siku za nyuma katika jitihada zako za kuleta maendeleo ya
kiuchumi na kijamii na ustawi wa nchi yako na wananchi wake.”
 Amesisitiza Rais Kikwete: “Wakati unajiandaa kuchukua
madaraka ya juu zaidi katika nchi yako, napenda kukuhakikishia
 msimamo wangu binafsi pamoja na ule wa Serikali yangu
wa  kuunga mkono Serikali yako. Ni imani yangu kubwa
 kwamba pamoja tutaweza kuendelea kusukuma mbele zaidi
 maendeleo ya nchi zetu – Kenya na Tanzania na pia utengamano
 wa Afrika Mashariki kwa manufaa ya nchi zetu na
wananchi wake.”
 

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB