RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KATIKA MAZISHI YA KOCHA ATHUMANI KILAMBO
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiondoka baada ya kuongoza maelfu ya
waombolezaji katika mazishi ya mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye
Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo Machi 11, 2013 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la
mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu
Athumani Kilambo leo Machi 11, 2013 katika makaburi ya Kisutu jijini
Dar es salaam. Marehemu Kilambo, ambaye alifariki jana usiku baada ya
kuugua saratani ya koo kwa takriban miaka miwili, atakumbukwa
kama beki imara wa Yanga na Kocha stadi wa Pan Africa ambaye
aliiwezesha Klabu hiyo kutwaa ubingwa wa taifa mwaka 1982. Pia
amefundisha nyota wengi wa kandanda nchini wakiwemo kina Kassim Manara, Adolf Richard,
Mohamed Mkweche, Juma Pondamali na wengineo wengi ambao walichezea Taifa
Stars kutokea Yanga na Pan.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na Katibu Mkuu wa
Yanga Lawrence Mwalusako katika mazishi ya mchezaji mkongwe wa Yanga na
baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo leo Machi 11,
2013 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. wengine toka
kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika. Ndugu Adam Malima, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Mhe Ranmadhani Madabida na kulia ni Mwenyekiti wa Yanga Bw. Yusuf Manji.PICHA NA IKULU