MAKAMU WA RAIS BENKI YA DUNIA AKUTANA NA WAZIRI WA FEDHA WILLIAM MGIMWA


Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia  kwa Bara la Afrika, Bw. Makhtar Diop kulia ,akiwa ameambatana na  Maafisa  Waandamizi kutoka Benki ya Dunia wakati wa mazungumzo na Waziri wa Fedha Mhe. William  Mgimwa hayupo kwenye picha.
Balozi wa Tanzania nchini Japan  Bi. Salome Sijaona kushoto akifuatiwa na Dk. Servacius B. Likwilile Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha akifuatiwa na  ni Mhe. Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa na  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa Omari walioko nyuma ni maafisa waandamizi  wa Tanzania Jijini Tokyo – Japan wakimsikiliza kwa makini Bw. Makhtar Diop, ambaye ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Bara la Afrika.
Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Mhe. Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa pamoja na maafisa kutoka Benki ya Dunia wakiendelea na majadiliano juu ya kuangalia uwezekano wa kuisaidia Tanzania ili iweze kendelea kiuchumi hapa Jijini Tokyo- Japan.
Kushoto kwa Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu ni Maafisa kwa Benki ya Dunia wakifuatilia kwa makini kuhusu mkutano huo wakiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania hapa Jijini Tokyo – Japan.
Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu akitoa maoni yake  kwenye mkutano na Makamu wa Rais wa Dunia hayupo pichani hapa Jijini Tokyo- Japan.
Wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini  majadiliano yaliyokuwa yakiendelea katika mkutano huo

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB