FREEMAN MBOWE AUNGURUMA JIJINI ARUSHA



Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh Freeman Mbowe akihutubia wananchi wa Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh Freeman Mbowe akihutubia wananchi wa Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha katika muendelezo wa kampeni za chama chake kuwania nafasi ya uwakilishi katika Halmashauri ya Jiji kupitia Kata hiyo. 
Mkutano huo nusura usifanyike hiyo jana baada ya kilichoelezwa kuwa chama hicho kilikosa eneo la kufanyia mkutano na hivyo kulazimiaka kufanyia nje ya ofisi za chama hicho Kata ya Daraja Mbili, ofisi ambazo ziko jirani na za mahasimu wao kisiasa, CCM.Aidha, ujio wa Mbowe haukujulikana mapema kiasi cha wananchi kushangaa kumuona jukwaani ghafla tu. Pia, Mh Mbowe hakuweza kumnadi mgombea wa chama hicho kwa kuelezwa kwamba alikuwa anashikiliwa na Polisi alikolazwa hospitali ya Mt Meru na hivyo kushindwa kuhudhuria mkutano huo.
SAM_5236
Godbless Lema nae akizungumza mkutanoni hapo.

SAM_5288
Juu na chini ni Sehemu ya umati wa watu uliojitokeza kusikiliza hotuba za viongozi wa Chadema. Katika mkutano huo, zaidi ya sh laki 3 zilichangwa na wananchi hao kusaidia kampeni zaidi za chama hicho katika Kata hiyo.
SAM_5296

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB