RAIS KIKWETE ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU ASKOFU THOMAS LAIZER WA KKKT








Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya leo, Alhamisi, Februari 14, 2013 ameungana na waumini wa Dayosisi ya Kaskazini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kuuaga mwili wa askofu wa jimbo hilo, Askofu Dkt. Thomas Laizer.
Rais Kikwete na ujumbe wake amewasili kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha kiasi cha saa 10:50 akaenda moja kwa moja kuaga mwili wa Marehemu Laizer na baadaye akakuta na kuwafariji wafiwa akiwamo Mke wa Askofu Laizer, Mama Maria Laizer.
Rais pia atashiriki mazishi yake yaliyopangwa kufanyika kesho, Ijumaa, Februari 15, 2013 katika Kanisa Kuu hilo la KKKT la mjini Arusha.
Askofu Dkt. Thomas Olmorijoi Laizer ambaye alizaliwa Machi 10, mwaka 1945 katika Kijiji cha Engarenaibor, Wilaya ya Longido, Mkoa wa Arusha alifariki dunia Alhamisi iliyopita, Februari 7, majita ya saa 12 jioni kwa magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la Damu.


Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB