MASWALI MENGI YAIBUKA KIFO CHA KAMANDA WA POLISI MWANZA

1. Endelea kufananisha picha. Lakini endelea pia kujenga mashaka kama nilivyoandika siku mbili zilizopita.

2. Kamanda alikuwa anatoka wapi - sherehe?

3. Alimbeba nani - mwalimu? Lifti? Kutoka wapi kwenda wapi? Mwalimu alikuwa anatoka wapi usiku huo? Hajaolewa? Mume wake yuko safari au alighairi sherehe? Mume wa mwalimu ni nani? Wanaishi wapi? Alimwacha wapi mume wake na kubebwa na polisi mkuu wa mkoa? Aliwaacha wapi aliokuwa nao na yeye kupata lifti? Kwanza kabisa, alikuwa na nani kabla hajapewa lifti. Mtu wa mwisho kumwona mwalimu na polisi wakiondoka ni nani? Kama polisi alipakia abiria wengine walishuka wapi?

4. Mkuu wa polisi na mwalimu walikuwa pamoja kwa muda gani wakiwa peke yao na wapi? A La Kairo au wapi? Hapo Kairo walikuwa wakifanya nini - tangu lini hadi lini? Mwalimu wa shule ya msingi ya Nyamagana, eti? Alikuwa anatoka wapi - naye kwenye sherehe hiyohiyo na Burlow?

5. Mwalimu mkuu anasema nini? Dada yake? Ndugu zake wengine? Hivi polisi mkuu wa mkoa na mwalimu walikutana kwa bahati mbaya? Tafuta. Tafuta. 

6. Mahali aliposhambuliwa mkuu wa polisi ni karibu na kwake au kwa mwalimu?
7. Endelea kujenga mashaka: Ofisa uhamiaji aliyenusurika yuko wapi katika sinema hii? Hajui lolote? Kati ya polisi mkuu na mwanamke, hakika hakuna pandikizi la kukamilisha sura ya sinema? Hakuna?????? Tafuta. kama lipo linaweza kuwa limewekwa na nani na kwa nini?

8. Katika miaka mitatu iliyopita: Angalia kesi mahakamani Mwanza. Hakuna nyingi zinazohusu polisi na nyendo zao katika maisha ya familia mbalimbali? Hii ishu ya Burlow yaweza kuwa moja ya hizo? Uliza mahakimu - wamelalia malalamiko kwa kuwa polisi wamelalia uchunguzi na ushahidi? Tafuta. 

9. Yuko wapi mke wa polisi mkuu? Hakwenda kwenye sherehe? Alikatazwa? Hakupenda? Alijisikia vibaya? Hayupo Mwanza? Yuko wapi.

10. SINEMA HII INAFANANA NA ILE YA UDAKU. SIYO! Acha vijana wafumue muone kitakachotoka kichakani. Na hicho ndicho mazoea, tabia na sasa utamaduni. 

11. Kumbuka Burlow alitoka mkoani Mara na mkondo wa wakimbizi na wahamiaji na utajiri wao, kama nilivyoeleza katika disipachi iliyopita, vina nafasi katika mahusiano na tabia za polisi na uhamiaji. Nani atajinyofoa katika hili lenya urefu na upana wa dunia.

12. Naomba Katu na wengine, mwendelee kuchimba. Kama kweli Burlow amefariki katika mazingira hayo, nasema kuna jambo ambalo halina nyumba maalum. Liko kila nyumba ya mwenye madaraka; mwenye fedha za nyongeza. Bali alale pale ambako Mwenyezi Mungu atapenda.
NDIMI:-
Ndimara Tegambwage
Information and Media Consultant
P.O. Box 71775, Dar es Salaam
Tel: 255 (0)713614872
e-mail: ndimara@yahoo.com
www.ndimara.blogspot.com
NAOMBA KUWASILISHA

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB