Skip to main content

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 NDANI YA JAMHURI MJI KASORO BAHARI MOROGORO



Pichani kulia ni Ofisa Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Simalenga akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh Joel Bendera ambaye ni mgeni rasmi ndani ya uwanja wa Jamhuri,wakati tamasha la Serengeti likiendelea kufanyika.
 Pichani mbele ni msanii Rich Mavoko akiliongoza kundi lake jukwaani.
 Ommy Dimpoz pichani kati sambamba na kundi lake wakitumbuiza kwenye jukwaa la Fiesta.

 Mkali wa R&B Ben Paul akiwaimbisha wakazi wa Morogoro waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,ndani ya uwanja wa Jamhuri.
Msanii wa bongofleva Linah akitumbuiza jukwaani.
Msanii mahiri katika mahadhi ya Mduara AT akiduarika na mmoja wa densa wake jukwaani.
Msanii muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Recho akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Jamhuri,mjini Morogoro,ambapo wakazi kibao wa mji huo (hawapo pichani) wamejitokeza kwa wingi.
Mmoja wa sanii chipukizi katika shindano la Serengeti Supa Nyota 2012, Ney Lee akionesha kipaji chake cha kuimba jukwaani.
Pichani juu na chini ni Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dayna na kundi lake la Wakali wa Classic wakitumbuiza jukwaani


Mkali wa Supa Nyota,Jo Meka akikamua jukwaani.
Mkali wa kusugua mangoma,Dj Zero akifanya makamuzi yake.

Mmoja wa wasanii chipukizi kutoka mjini Morogoro akitumbuiza kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012
Msanii chipukizi kutoka nyumba ya vipaji,THT,Alini Nipishe akiimba na shabiki wake jukwaani wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea.
Michael Jackson wa Morogoro akionesha umahiri wake kuchenza nyimbo za The Wacko Jacko.

Mmoja wa wasanii chipukizi kutoka mjini Morogoro akiimba jukwaani.

Wadau wa tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya uwanja wa Jamhuri.

 
 

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB