Mji wa Kismayo unakaribia kutekwa

Wanajeshi wa Kenya wakipambana na Al-Shabaab

Msemaji wa jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir anasema kuwa wanakaribia kuuteka mji wa bandarini wa Kismayo.
Meja Chirchir amekariri kuwa wapiganaji wa Kenya wanaopigania kundi la Al Shabaab ikiwa wataweza kujisalimisha watasamehewa
Kumekuwa na ripoti kuwa wapiganaji wa al-Shabaab wamenza kuutoroka mji huo katika siku chache zilizopita baada ya kuzingirwa na majeshi ya muungano wa Afrika kutoka pande zote
Mji huo ndio ngome ya mwisho ya Al-Shabaab, ambayo huitumia kwa kuingza silaha na zana za kivita kutoka nchi za kigeni.
Muungano wa Afrika unasema kuwa wanajeshi wa Somalia wameuteka mji wa Janaa Cabdlla ngome nyingine ya wapiganaji hao iliyo umbali wa kilomita hamsini Magharibi mwa Kismayo
BBC SWAHILI

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB