LEMA :SEREKALI ISITUGOMBANISHE CHADEMA NA WAMACHINGA ARUSHA
Aliyekuwa mmbunge wa jimbo la arusha mjini Godbless Lema kulia akiwa anaongea na waandishi wa habari kushoto kwake ni aliyekuwa mwanachama wa chama cha mapinduzi ambaye alijivua gamba nakuamia chadema James ole milya ,huku katika kati ni Katibu wa mkoa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Gulkugwa Amani wakati wa mkutano wa waandishi wa habari na viongozi wa chama hicho uliohusiana na kuhairisha kwa mkutano uliokuwa ufanyike jana.
James ole milya akiongea katika mkutano huo ambapo alisisitiza na kuitaka serekali irejeshe viwanja vyote vya michezo vinavyomilikiwa na CCM kwani viwanja hivyo vimejengwa kwa kutumia fedha za wananchi na sio za chama hicho ,ambapo alitaja baadhi ni pamoja na kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid,Nyamagana kilichopo mwanza pamoja na kiwanja cha CCM kirumba
Katibu wa mkoa wa chama cha demokrasia Gulkugwa Amani na maendeleo chadema akiwa anasisitiza jambo wakati wa mkutnao wao na waandishi wa habari
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Bw Goodbless Lema amemtaka
Mkuu wa Willaya ya Arusha Mjini Bw John Mongela kuhakikisha kuwa
anatumia busara zaidi ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Arusha
kupitia kwa Mkuu huyo wamegeuza matumizi ya uwanja ambao ulikuwa
unatumiwa na CHADEMA kwa ajili ya mikutano ya nje na kuwapa eneo hilo
wa Machinga siku moja kabla ya kufanya mkutano wa hadhara.
Bw Lema aliyasema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari
mara baada ya chama hicho kushindwa kufanya mkutano wa hadhara katika
viwanja vya NMC ambavyo vimegeuzwa kwa ajili ya matumizi ya Wamachinga
Aidha Bw Lema alifafanua kuwa kitendo hicho cha kubadilishiwa matumizi
ya uwanja ambao ulikuwa ukitumiwa sana na Chadema umefanywa na Mkuu wa
Wilaya ya Arusha na hayo yote yanatokana na chuki binafsi za maslahi
ya kivyama ingawaje bado chama hicho kina uwezo mkubwa sana wa
kuendelea kufanya kazi yake
Alifafanua kuwa hali hiyo ya kubadilisha matumizi ya uwanja kutoka
uwanja wa matumizi ya kijamii na kwenda kwenye uwanja wa kuuza vitu
kwa wafanyabiashara wadogo wadogo(MACHINGA) umetokana na chuki ambazo
zilikuwa zimeelekezwa kwa chama hicho dhidi ya wamachinga hali ambayo
imetokana na chuki za siasa hasa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha
“inaamanisha nini leo tumeshapanga kufanya mkutano alafu Mkuu wa
Wilaya anaelekeza watu wamwage Vifusi kwa ajili ya eneo la Machinga je
wakati wote huo walikuwa wapi na kama sio kutogombanisha na Machinga
ninini lakini bado tuna nafasi kubwa sana ya kuendelea kufanya
mikutano hata kama ni nyumbani kwetu na tutawatetea hawa vijana ambao
ni machinga kufa na kuzikana”aliongeza Bw Lema
Pia aliishauri Serikali kuhakikisha kuwa kabla hawajafikiria kuwatoa
wafanyabaishara wadogowadogo (MACHINGA)wanatakiwa kutengeneza
miundombinu imara ambayo itatumika lakini kwa sasa ndani ya eneo hilo
ambalo limegeuzwa matumizi yake na Mkuu wa Wilaya bado walengwa
watapata shida sana na kutokana na hali hiyo hata uchumi nao
utadidimia sana
“ukingalia sana ndani ya viwanja hivi vya NMC ambavyo vilikuwa
vikitumika na Chadema na sasa ni viwanja vya machinga bado ni hafifu
sana kutokana na kuwa hakuna miundombinu yoyote alafu pia kabla hawa
watu hawajapelekwa kule walitakiwa kuhakikisha kuwa wanaboresha ila
wamewakimbizia huko kwa ajili ya mkutano wetu ambao ulikuwa wa
kuchakaza sura ya Arusha kutokana na ukweli ambao sisi
tunaujua”aliongeza Bw Lema
Awali Katibu wa chama hicho kwa mkoa wa Arusha bw Amani Golugwa
alisema kuwa mbali na hayo wamejipanga kuhakikisha Mji wa Arusha
unakuwa na historia yake kwa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata
haki yake ya msingi na wala sio kuonewa na baadhi ya viongozi ambao
hawana maadili ambao ndio chanzo kikubwa sana cha umaskini.