Serengeti Fiesta 2012 Dodoma funika mbayaaaa!!!


Msanii wa muziki wa kizazi kipya,mahiri katika miondoko ya miduara,AT akimrusha kimduara duara shabiki wake jukwaani huku shangwe za hapa na pale zikiwa zimetawala kutoka kwa watazamaji.

Wasanii mahiri wa filamu hapa nchini nao walikuwepo kuliunga mkono tamasha la Fiesta ndani ya Dodoma,kutoka kulia ni Jacob Steven a.k.a JB,Wema Sepetu pamoja Aunt Ezekiel.
Ray Kigosi akilicheza sebene jukwaani.
Ray akimtambulisha Wema Sepetu kwa mashabiki.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh.Dr Rehema Nchimbi akisoma jina la mshindi wa gari aina ya Vitz inayotolewa na kampuni ya Push Mobile,ikiwa ni sehemu ya mchakato wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,pichani kati ni Meneja masoko wa kampuni ya Push Mobile,Rodney Lugambo,Muwakili shi wa michezo ya bahati nasibu ya Taifa,Bwa.Humudi pamoja na Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini,Mh Lephy Gembe. 
 Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini,Mh Lephy Gembe akiwasalimia wakazi wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi  kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,kwenye uwanjawa jamuhuri.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah kutoka THT akitumbuiza jukwaani wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 
 Msanii wa bongofleva aitwaye Shetta akiwaimbisha washabiki wake
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Rich Mavoco akiwaimbisha washabiki wake kibao waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lililofanyika ndani ya uwanja wa Jamuhuri.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Dayna akijitokeza kwa mbwembwe jukwaani  kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma,ambapo wakazi wake wamejitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wanaotumbuiza kwenye jukwaa hilo.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB