MONGELLA ATUNUKIWA TUZO YA UMAHIRI AFRIKA

mongella01bc
Mhe Balozi Getrude Mongella
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia M. Simba amemkabidhi tuzo ya umahiri katika uongozi Mhe Balozi Getrude Mongella kutokana na juhudi zake katika kuwakomboa wanawake wa Bara la Afrika.
Hafla ya kukabidhi Tuzo hiyo ya miaka 50 ya Pan African Women’s Organization (PAWO) ilimefanyika leo (23/12/2013) Courtyard Hotel jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi wa Wizara waliongozwa na Katibu Mkuu Bibi Anna T. Maembe na kushirikisha wajukuu wa Balozi Mongela.                          
                  Mhe. Sophia Simba alifafanua kuwa lengo la hafla hiyo ni kutambua utumishi wake na kumkabidhi Mheshimiwa Mongella Tuzo ya heshima ya Wanawake Mashuhuri Barani Afrika ambao walionesha uongozi uliotukuka katika kutetea umoja, haki na usawa wa wanawake. Awali tuzo hiyo ilitolewa katika Mkutano maalumu wa Mawaziri wa Wanawake na Jinsia uliofanyika Pretoria, Afrika Kusini mwezi  Agosti 2-13, 2013. Aidha, Wizara imetambua umuhimu wa kujulisha taifa kuhusu mchango wa Balozi Mongella na kutokana na uzoefu wake uliosaidia ukombozi wa wanawake wa Barani Afrika.
Itakumbukwa kuwa Mhe. Mongella alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano wa Wanawake uliofanyika Beijing Nchini China mwaka 1995.  Matokeo ya Mkutano huo ni maandalizi ya Azimio na Ulingo wa Beijing, ambao uliainisha maeneo 12 ya kimkakati ambayo utekelezaji wake umesaidia kuleta usawa wa kijinsia na wanawake kupatiwa haki zao. Nchi ya Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa inatekeleza maeneo hayo muhimu ikiwa ni pamoja na elimu na mafunzo, afya, ajira, uwezeshaji kiuchumi, usawa, kushiriki uongozi na maamuzi na kuzuia ukatili wa kijinsia nk.
Akiwa Rais wa Bunge la Afrika Mhe. Mongella alitumia nafasi hiyo kuelimisha na kutetea maslahi ya wanawake Barani Afrika. Aidha, amekuwa akishiriki kikamilifu katika mikutano mbalimbali inayohusu maendeleo ya Wanawake na jinsia katika ngazi ya kikanda. Katika ngazi ya kitaifa Mheshimiwa Mongela ametumikia nyadhifa mbalimbali kama vile Waziri, Mbunge, na amekuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wanawake hapa nchini.
Simba alisisitiza kuwa Mheshimiwa Mongella amesimama kidete kutetea maslahi ya wanawake, jambo ambalo linamfanya kuwa mfano wa kuingwa na wanawake wote wa kitanzania  maana ametenda kwa uthabiti na leo tunajivunia  uzoefu wake.
Akitoa shukurani zake Mheshimiwa Balozi Mongella alikumbusha kuwa chanzo cha kuanzishwa kwa Pan African Women’s Organization ni Tanzania (PAWO). Na kwamba ilianza mapema hata kabla ya kuanzishwa kwa vuguvugu la Umoja wa Nchi za Afrika (OAU). Changamoto kubwa ni kwamba kutothamini ubunifu wetu wenyewe kumesababisha PAWO kulegalega. Hafla hii inatukumbusha kuthamini michango ya wazalendo ili kusisimus fikra zenye manufaa katika jamii. Njozi ya Balozi Mongella ni kuona kuwa watoto wa kike wanapatiwa haki ya elimu ili kuzalisha akina -Mongella wengi nchini. Aidha, vijana wameaaswa kuwa na maadili na kuepuka matusi ya waziwazi katika kutafuta nafasi za uongozi jambo linalovunja heshima na utu.
Habari Na Erasto ching’oro- Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB