VIJANA WEKENI MSISITIZO MASOMO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA ILI MUWE WAJUZI NA KULETA MAENDELEO NCHINI

PIX 1Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mh Benjamin William Mkapa akizungumza na wanasayansi vijana katika mkutano wa wanasayasi vijana uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.PIX 2Baadhi ya wanasayansi wakiwa katika mkutano wa wanasayasi vijana uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………….
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
Vijana nchini hawanabudi kupenda kujifunza masomo ya Sayansi na teknolojia ili waweze kupata ujuzi na mitazamo katika sekta ya gesi ambayo inakuwa kwa kasi kubwa hapa nchini na Duniani kwa ujumla.
Kiukweli sayansi na teknolojia inasadikiwa kuwa mihimili mikubwa ya sasa katika kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali kwani mambo mengi yenye kuhitaji haraka hutegemea sayansi na teknolojia kwa kiasi kikubwa.
Licha ya kuwepo kwa changamoto zinazozikabili baadhi ya nchi nyingi za Afrika katika kupata maendeleo ikiwa ni pamoja na kutowekeza katika sayansi na teknolojia, hali inayopelekea baadhi ya nchi nyingi kukosa Wataalam wa kutosha katika mambo ya sayansi na teknolojia, hivyo nchi za Afrika zinahitaji kujikwamua na changamoto hiyo kwa kuhakikisha kuwa zinawekeza katika sayansi ili kubadilisha uchumi wa Afrika.
Sayansi na teknolojia hapa duniani huleta maendeleo makubwa hivyo Vijana wanatakiwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujituma katika mambo ya sayansi na teknolojia ili kuweza kuleta uchumi endelevu.
Sambamba na hilo, katika Kongamano liloandaliwa hivi karibuni na Wizara ya Nishati na Madini nchini Tanzania ambao ulifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal ambao ulikuwa ni mkutano wa tatu wa Wanasayansi Vijana Duniani wenye lengo la kuhakikisha kuwa vijana wanashiriki vyema katika rasilimali za duniani kwa ajili ya maendeleo na ukuaji wa uchumi thabiti, Wakala wa Jiolojia nchini, Profesa Mruma alisema kuwa Mkutano huo una lengo la kurithisha taaluma ya jiolojia inayohusisha madini, rasilimali, gesi na mafuta kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.
Kongamano hilo la Vijana liliwakutanisha vijana toka nchi zaidi ya 42 zikiwemo baadhi ya nchi za Afrika Tanzania ikiwemo na ambaye ndiyo alikuwa mwenyeji wa Kongamano hilo.
Katika kongamano hilo, Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na madini, Mhe. Masele alisema kuwa Serikali ya Tanzania imewekeza nguvu zake kwa katika kuendeleza sayansi ya mambo ya gesi na mafuta pamoja na afya kwa kuanzisha Vyuo mbalimbali na kuwapeleka baadhi ya Watanzania kwenda kusoma nje ya nchi ili waweze kupata ujuzi na kuwa wataalam na wakaguzi katika sekta ya gesi, mafuta na afya kwa lengo la kuja kuisaidia nchi.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB