Viongozi wanapogongana Ziarani - Mbowe na Ole Medeye Uso kwa Uso Bomang’ombe


photoMwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye. Viongozi hao walikutana juzi eneo la Bomang'ombe, wilayani Hai, kila mtu akiwa katika ziara yake. Wakati Mbowe alikuwa anaendelea na ziara ya kuzungukia wananchi katika vijiji mbalimbali jimboni kwake Hai, Medeye alikuwa katika ziara yake binafsi maeneo ya jimbo hilo.

Ziara ya Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai katika picha, akikagua ujenzi na uhai wa chama (Chadema) ngazi ya misingi/vitongoji ambapo anakutana na kuzungumza na viongozi wa misingi hiyo.
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Hai, akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa chama hicho Kijiji cha Mtakuja, Mzee Ally Mbatia. Mbowe yuko katika ziara ya kukagua uhai na kuimarisha ujenzi wa chama katika ngazi ya chini kabisa ya chama hicho, msingi, kwenye maeneo ya vitongoji mbalimbali katika vijiji vya Jimbo la Hai
Picha na Tumaini Makene

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB