MHESHIMIWA WILLIAM LUKUVI KWENYE ZIARA LONGIDO ARUSHA
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Williama Vangimembe Lukuvi jana alifungua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido na kuwataka wananchi kununua nyumba hizoili NHC iweze kujenga zingine kusaidia Wilaya hiyo kupata makazi bora. Picha zote na Muungano Saguya- Longido, Arusha
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akikagua maandalizi ya ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido, Arusha kabla ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi kufanya ufunguzi huo jana.