ALI HASSAN MWINYI MGENI RASMI TAMASHA LA PASAKA MWAKA HUU

indexRAIS Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ameombwa kuhudhuria kwa mara nyingine katika Tamasha la Pasaka linaloadhimisha miaka 15 mwaka huu.
Mwinyi ndiye mgeni muasisi  wa tamasha hilo ambako kwa mara ya kwanza alikuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la mwaka 2000.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama anapenda rais huyo mstaafu ahudhurie siku hiyo kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi muasisi ambaye pia ni mlezi, hivyo akihudhuria atajionea maendeleo yake.
“Nitapenda sana iwapo rais Mwinyi atahudhuria siku ya Tamasha ili aweze kushuhudia muendelezo wa Tamasha tangu alipolizindua mwaka 2000,” alisema Msama.
Alisema hadi sasa maandalizi yamekamilika hivyo mashabiki wa nyimbo za injili wakae mkao wa kula wakisubiria tamasha hilo mapema mwanzoni mwa mwezi ujao.
“Mashabiki wakae tayari maandalizi yamekamilika, tunachosubiri ni siku yenyewe ifike, waimbaji maarufu watakuwepo wakisufu na kuabudu, hivyo ni wakati wenu mzuri wa kwenda kupata neno la Mungu kwa njia ya uimbaji,” alisema.
Tamasha hilo la kimataifa litakalobeba waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili ndani na nje ya nchi litafanyika mwezi ujao Dar es salaam na baadae kwenda katika baadhi ya mikoa.
Waimbaji watakaohudhuria Tamasha hilo ni pamoja na Jessica Honore,  Joshua Mlelwa, Upendo Nkone, Kwaya ya Kijitonyama na  John Lisu.
Kwa upande na waimbaji kutoka je  ya Tanzania atakuwepo Rebecca Malope na Solly Mahlangu (Afrika Kusini), Faustin Munishi (Kenya).

Popular posts from this blog

MH. AMANI ABEID KARUME AFUNGUA SKULI YA DONGE ZANZIBAR