MH. LOWASSA ASHIRIKI IBADA YA SIKUKUU YA KRISMAS VISIWANI ZANZIBAR


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa na mkewe Mama Regina Lowassa wakiungana na Wakristo wengine kwenye ibada ya Sikukuu ya Krismas iliyofanyika juzi kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe Zanzibar.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa salaam za Xmas kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Mwanakwerekwe Zanzibar mara baada ya ibada ya Sikukuu hiyo juzi.Mh. Lowassa yuko visiwani humo kwa mapumziko ya sikukuu hiyo,ambapo amewataka watanzania kusherehekea sikukuu hizi za krismas na mwaka mpya kwa amani na upendo huku tukilinda umoja na mshikamano uliojengwa na waasisi wetu Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB