HII HAPA TREIN YA KISASA ALIYOZINDUA RAIS KIBAKI MJINI NAIROBI.
Trein ya kisasa iiliyozinduliwa Kenya inavyoonekana kwa ndani.
Viongozi wakenya katika uzinduzi wa Trein mpya
Rais Kibaki ikiteremka katika Trein mjini Nairobi
Treni
ya kwanza ya aina yake imezinduliwa tangu Kenya kujipatia uhuru mwaka
1963. Rais Kibaki aliyefungua rasmi kituo cha Syokimau na alikuwa
miongoni mwa watu wa kwanza kuipanda treni hiyo.
Kituo
cha treni cha Syokimau ni cha kwanza cha aina yake nchini Kenya, kikiwa
na mashine za elektroniki zinazokagua vyeti vya usafiri, pamoja na
skirini kubwa ambazo zinatangaza safari za treni. Kila behewa lina uwezo
wa kubeba abiria sabini pamoja na miamoja na ishirini watakao simama.
Treni
hiyo inanuiwa kupunguza msongamano wa magari mjini Nairobi ambao ni
mojawapo ya miji unaokuwa kwa kasi barani Afrika ukiwa na watu zaidi ya
milioni tatu.