MAMA SALMA KIKWETE ZIARANI MKOANI RUKWA
Mama Salma Kikwete (MNEC) Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Tanzania (WAMA) akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Rukwa mara baada ya kushuka katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga leo. Anaemuongoza ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Mama Salma akiveshwa Skafu na moja ya Skauti mara baada ya kuwasili Mkoani rukwa.
Mama Salma akifurahi na vikundi vya ngoma. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Mama Salma akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Mkoa wa Rukwa Aeshi Hillal ambae pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini CCM. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kwela Ignas Malocha.
Mama Salma Kikwete akijadili jambo na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya katika Ikulu ndogo ya Sumbawanga Mkoani Rukwa leo mara baada ya kuwasili katika ikulu hiyo kwa ajili ya mapumziko mafupi, chakula na kusomewa taarifa ya Mkoa.
Mama Salma Kikwete Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitaka ufafanuzi wa jambo kutoka Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya wakati akimsomea taarifa ya Mkoa wa Rukwa katika sekta ya afya.
Kutoka kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima, wa tatu ni Ndugu Aeshi Hillal Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Mkoa wa Rukwa, Iddi Kimanta Mkuu wa Wilaya ya Nkasi na Mussa Chang’a Mkuu wa Wilaya ya Kalmbo wakifuatilia taarifa hiyo iliyokuwa ikiosmwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Mganga Mkuu Hospitali Kuu ya Mkoa Rukwa Dkt. Gurisha Richard akifafanua jambo kwa Mama Salma Kikwete juu ya vifo vya mama na mtoto Mkoani Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa InjiNIA Stella Manyanya akimkabidhi Mama Salma Kikwete taarifa hiyo ya Mkoa wa Rukwa kuhusu sekta ya Afya. Katika taarifa hiyo Mama Salma kikwete aliutaka uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuendelea kutoa elimu kwa kina mama kabla na baada ya kujifungua ili kupunguza vifo vya mama na mtoto ambavyo vingi husababishwa na uelewa mdogo wa akinamama juu ya afya zao na watoto.