MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA RASMI MRADI WA UPANUZI WA BARABARA YA KILWA, MBAGALA RANGI TATU



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakati alipowasili katika hafla ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu . Katikati ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (kushoto) wakishiriki kwa pamoja kukata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakifunua kitambaa kwa pamoja ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu . Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na kumpongeza Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, mara baada ya balozi huyo kumaliza kusoma hotuba yake iliyochanganywa na Kiswahili, wakati wa hafla ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu . Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli.
 Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Masaki Okada, akishiriki kucheza sebene la bendi ya Msondo Ngoma na Vijana wa kikundi cha uhamasishaji cha Temeke, wakati wa hafla hiyo.
 Baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma, wakishambulia jukwaa kutoa burudani wakati wa halfa hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wazee wastaafu wa CCM, mara baada ya kumaliza kupiga nao picha ya pamoja ya kumbukumbu wakati wa hafla ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi kutembea na kukagua sehemu ya Barabara ya Kilwa eneo la Mbagala Rangi tatu, baada ya kufungua rasmi barabara hiyo iliyokamilika kwa Upanuzi na ukarabati.  Picha na OMR

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB