KINANA AKIHUTUBIA MAELFU YA WATU GEITA JIONI HII


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa mpira, mjini Geita mkoani Geita, jioni hii, akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya mikoa minne kujitambulisha kwa wanachama na kukagua uhai wa chama ngazi za mashina na matawi na kusimamia na kueleza utekelezaji wa ilani ya Chama. (Picha na Bashir Nkoromo)
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi leseni za wachimbaji wadogo machimbo ya Mugusu, Geita, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mkoani Geita. Jumla ya leseni 21 zilikabidhiwa kwa wachimbaji hao baada ya kutolewa na serikali ili kuwwezesha wachimbaji wadogo nao kunufaika na m,adini badala ya wachimbaji wakubwa tu.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizindua shina la wakereketwa wa CCM la wajasiriamali watengeneza fenicha katika mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, jana. Nape aliwapa pia ,msaada wa sh. milioni moja kwa ajili ya wajasiriamali hao kukuza shughuli zao.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtuza msanii, Kasim Magembe, baada ya kuridhishwa na uhodari wake alipotumbuiza kwenye mkutano wa CCM uliofanyika uwanja wa Mpira, Geita leo
Nape Nnauye akisalimia vijana mbalimbali katika mji wa Geita mkoani Mwanza.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB