WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWASILI MKOANI KATAVI TAYARI KWA UZINDUZI RASMI WA MKOA HUO


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutegwe mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda leo mchana kwa ajili ya kushiriki katika shughuli ya uzinduzi rasmi wa mkoa huo, utakaofanyika siku ya jumapili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda, mkoa huo utazinduliwa rasmi kwa ving’ola na Mh. Dkt. Gharib Bilal Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania anayetarajiwa kuwasili kesho mjini Mpanda tayari kwa ajili ya uzinduzi huo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda viongozi mbalimbali wa CCM baada ya kuwasili mkoani Katavi leo mchana  katikati ni Waziri wa Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rtengwe.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi (Chadema)  mara baada ya kuwasili mjini Mpanda leo
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe kwa ajili ya kukagua vikundi vya ngoma katika uwanja wa ndege wa Mpanda mara baada ya kuwasili, kushoto ni mke wake mama Tunu Pinda.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda kushoto akifurahia jambo na Dkt. Mary Nagu waziri wa Uwezehaji Ofisi ya Waziri Mkuu wakati walipowasili katika uwanja wa ndege wa mpanda leo mchana.
Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda akuwapungia mkono wakazi wa mjini Mpanda waliofika uwanja wa ndege kumlaki , kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda katika uwanja wa ndege wa Mpanda.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa MpandaMjini, Said Arfi (Chadema) wakati wa  mapokezi ya waziri kuu Mizengo Pinda mjini Mpanda, Mh. Rajab Rutengwe anatoa kauli mbiu yake kuwa “SIASA NI MAENDELEO”.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajabu Rutengwe akimsiliza Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi kamanda Dhahiri Kidavashari wakati akimpa maelezo ya utaratibu wa mapokezi ya mgeni huyo, kulia anayesikiliza kwa makini ni Afisa Habari wa mkoa wa Rukwa Bw. Hamza Temba
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Mkoa wa Rukwa ili kupata maelezo kadhaa katika maonyesho hayo kulia ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo katika banda la mkoa wa Rukwa katikati  ni Mke wake Mama Tunu Pinda.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa maafisa wa ardhi katika mkoa wa Katavi mara baada ya kutembelea banda la mkoa huo.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB