ZITTO KABWE 'AANIKA' UTAJIRI WAKE



Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Kabwe amejibu tuhuma zinazoelekezwa kwake kwa kusema "Sijawahi kuwa na nyumba wala kiwanja hapa Dar wala Dodoma isipokuwa nyumbani Kigoma, huko nina nyumba vya vyumba viwili tu ambayo niliijenga wakati wa uchaguzi baada ya wazee kunishauri kuwa siyo vizuri kuendelea kutumia nyumba ya baba yangu. 
 Ninapaswa kuwa na kwangu. Labda kuna shamba la hekari tatu na nusu nililopewa na bibi yangu liko Kigamboni eneo la Mbutu, sijaendeleza hadi sasa, lipo tu. Lakini pia ieleweke kuwa nina uwezo wa kujenga kama Mbunge, wabunge wenzangu wengi tu wanajenga, mimi ninashindwa kwa sababu ya majukumu yangu ya kifamilia. Nimeshasikia sana watu wanazungumza ninajenga ghorofa kubwa Dodoma na baadhi ya watu wanaiita sehemu hiyo kuwa ni kwa
Zitto sina hata kiwanja Dodoma, uzushi mtupu wa maadui zangu kisiasa". 

Akizungumzia Utitiri wa magari ya kifahari anayodaiwa kuwa nayo anasema "Watu wanaishi maisha ya kufikirika sana, hayo magari wanayodai ninayo sina, iko hivi; mimi nina gari moja dogo aina ya Toyota Vista na nina Land Rover, Free Lander ambalo nimelichukua kwa mkopo, bei yake ni Dola 30,000, sijamaliza kulipa. Hayo mengine yanayosemwa ninayo ni ujinga tu wa watu. 
Baada ya kuwa mbunge, nakumbuka April 2007 niliingiza nchini gari aina ya Hammer na nadhani nilikuwa mtu wa pili kuingiza gari hilo hapa nchini. Kaka yangu Salum anayefanya biashara ya magari ndiyo aliyeniletea na hili sikuliendesha zaidi ya wiki mbili, likanishinda. Lilikuwa la kifahari mno, nikamwambia alichukue aliuze na hela yangu anirudishie. 

Nakumbuka nilikwenda nalo Dodoma nikiwa naendesha na nilikwenda na Dk. Slaa na siku moja mwenyekiti wangu Mbowe baada tu ya kuletewa tukiwa Protea Hotel iliyo karibu na Kanisa la mtakatifu Petro, alijaribu kuliendesha akaniambia ni gari zuri sana. Hili nililikataa. Mwaka 2008 nilinunua Toyota Land cruiser V8. Hili nililitumia hadi kwy kampeni mwaka 2010 na baada ya hapo nililiuza. 

Salum alipoona sina gari kwa sababu nadhani ya kujua mimi ni mbunge akaniletea tena Range Rover Vogue Sport nililitumia kidogo likanishinda kwa sababu ni la kifahari sana, sikuweza kuligharamia. Nina akaunti mbili tu moja benki ya NMB na nyingine benki ya CRDB na zote hazina fedha zaidi ya shs Mil. 15 kila moja."- Zitto Kabwe

williammalecela.blogspot.com

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB