MWIGULU NCHEMBA AUNGURUMA ARUSHA UCHAGUZI WA UDIWANI

Mh.Mwigulu Nchemba akipokewa na wanachama wa CCM waliojitokeza viwanja vya Shule ya Msingi Erelai kata ya Erelai mkoani Arushahii leo wakati wa kampeni za kumnadi Mgombea Udiwi kwa tiketiYA CCM Mwalim Emanuel Laizer

Meya (kushoto)wa wilaya akiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya wakati wa mkutanohuo viwanja  vya shule ya msingi Erelai ARUSHA.

Mamia ya wananchi wakisikiliza sera za Mgombea wao pamja na hotuba ya Mh.mwigulu Nchemba.

Naibu katibu mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba akiomuonesha moja ya vijana waliojeruhiwa kutokana na siasa chafu za vyama vya upinzani.hapa Mwigulu anasisitiza siasa zio vita.Siasa ni amani na utulivu wapuziwe wote wanaohamasisha vurugu hapa nchini


Makada wa CCM Juliana shonza na Mtela mwampamba wakifuatilia mkutano huo kwa karibu.

Huyu ndiye mgombea wa Udiwani kata ya erelai Arusha mjini.Ndugu Mwalimu emmanuel Laizer.Mgombea huyu kwa tioketi ya CCM ameomba apewe kura za kutosha iliawaletee maendeleo wanakata ya Erelai.Amesisitiza ameshaanza kufuatilia miradi ya madarasa 4 ya shule ya sekondari elerai pia mradi wa maji upo unaelekea kumalizika.

Mamia ya watu hasa wanachama wa CCM walijitokeza kwenye mkutano huuo kusikiliza sera za chama chao.Katika moja ya mambo ambayo Mh.Mwigulu chemba amewaomba wananchi hawa ni kutovipa nafasi vyama vinavyoshabikia uvunjifu wa amani..

Naibu katibu mkuu wa CCM Mh.mwigulu Nchemba akimnadi mgombea udiwani wakati wa mkutano huo hii leo.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB