Rais Dkt. Kikwete afungua ubalozi wa Heshima San Francisco

0L7C0006
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi ofisi ya ubalozi wa heshima(Honorary Consulate) wa Tanzania jijini San Francisco nchini Marekani leo jioni.Kulia ni Balozi wa heshima wa Tanzania jijini San Francisco Mh.Ahmed Issa na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula na wapili kushoto ni Mke wa Balozi Mama Sherry Julin Issa. 0L7C0085Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima wa Tanzania jijini San FranciscoMh.Ahmed Issa,(wapili kushoto) muda mfupi baada ya kufungua ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini San Francisco nchini Marekani leo jioni.Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula na kulia ni mke wa balozi Ahmed Mama Sherry julin Issa. 0L7C0220
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio jijini San Francisco Marekani muda mfupi baadaya kufungua ubalozi wa heshima wa Tanzania na kuzungumza nao leo jioni. 0L7C0310
Rais Dkt.Jakaya MrishoKikwete akizungumza na baadhi ya Watanzania waishio jijini San Francisco Marekani leo jioni.Rais Kikwete yupo nchini Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine atahutubia kikao cha 68 cha Umoja wa Mataifa Jijini New York Marekani(picha na Freddy Maro)

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB