MAMA SALMA AZINDUA KISIMA CHA MAJI KATIKA HOSPITALI YA SEKOU TOURE JIJINI MWANZA


IMG_3758  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi kisima cha maji kilichochimbwa katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure,kwa msaada wa Kampuni ya Bia ya Serengeti. Kisima hicho kimegharimu shilingi milioni sabini. wa pili kulia  ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndugu Paschal Mabiti na kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Jaji Mark Bomani na wamwisho kulia ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela. Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 7.3.2013.(PICHA NA JOHN LUKUWI)
IMG_3777Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua koki ya maji wakati wa kuzindua rasmi kisima cha maji katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure .
IMG_3782Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisaidiana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr. Valentino Bangi  kumtwisha ndoo ya maji ndugu Getrude Ndaweka ambaye ni afisa muuguzi katika hospitali ya Sekou Toure wakati wa sherehe za uzinduzi wa kisima cha maji hospitalini hapo tarehe 7.3.2013.
IMG_3833Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikewte akimjulia hali mtoto Juma Joseph, 6 , kutoka katika kijiji cha Karumo, wilayani Sengerema aliyelazwa katika hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria`.
IMG_3881 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wafanyakazi na wananchi wa jiji la Mwanza waliohudhuria shaerehe ya kuzindua kisima cha maji katika hospitali ya Sekou Toure tarehe 7.3.2013.
IMG_3972Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikewte akiwahutubia mamia ya wafanyakazi na wananchi wa jiji la Mwanza baada ya kuzindua rasmi kisima cha maji katika hospitali ya Sekou Toure tarehe 7.3.2013.
IMG_3747
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akifungua kitambaa na baadaye akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi kisima cha maji kilichochimbwa katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure,kwa msaada wa kampuni ya bia ya serengeti. Kisima hicho kimegharimu shilingi milioni sabini. Kushoto kwa mama ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndugu Paschal Mabiti na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Jaji Mark Bomani na wamwisho ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr. Valentino Bangi. Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 7.3.2013.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB