MAMA ASHA BILAL MGENI RASMI TUZO ZA MWANAMAKUKA KATIKA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

2BMke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwahutubia wanawake na wageni waalikwa katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, zilizofanyika sambamba na uksherehekea siku ya Wanawake Duniani, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana Machi 8, 2013. Picha na OMR03BMke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya hundi ya Sh. milioni 6, mshindi wa kwanza wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, Aziza Mbogolume, wakati wa hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika sambamba na kusherehekea siku ya Wanawake Duniani, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
3BMke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, na baadhi ya wageni waalikwa wakishiriki kucheza muziki na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Baby Husna, wakati akitoa burudani kwenye hafla ya kutoa tuzo za Mwanamakuka 2013 zilizofanyika sambamba na sherehe za siku ya Wanawake Duniani, katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana Machi 8, 2013. Picha na OMR5BWashiriki wa onyesho la mitindo ya mavazi ya Mwanamakuka, wakipita jukwaani wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Tuzo za Mwanamakuka 2013, ambapo zawadi hizo zilikabidhiwa na Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, jana Machi 8, 2013 katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
6BMaadam Ritah Paulsen akishiriki katika kuonyesha mavazi wakati wa hafla hiyo.7B8BMama Asha Bilal, akishiriki pamoja na wageni waalikwa kuburudika kucheza muziki wa kizazi kipya wa Msanii Q-Chilla, wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Mwanamakuka zilizofanyika sambamba na sherehe za siku ya Mwanamke Duniani, jana Mchi 8, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na OMR9BMke wa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wadhamini waliofanikisha kufanyika kwa hafla hiyo ya utoaji tuzi za Mwanamakuka 2013, baada ya kukabidhi tuzo hizo kwenye hafla hiyo iliyofanyika jana machi 8, 2013 kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB