Posts

VIFARANGA 5000 VYACHOMWA TANZANIA

Image
Tanzania kwa mara nyengine tena imechoma vifaranga 5,000 vya kuku vinavyodaiwa kuingizwa nchini humo kupitia mpaka wa Kaskazini wa Namanga kutoka Kenya. Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya, katibu katika wizara ya mifugo nchini Tanzania Maria Mashingo, amesema kuwa mfanyibiashara aliyeingiza vifaranga hao nchini Tanzania hakuwa na vibali vinavyohitajika . Tanzania imesema kuwa hatua ya kuwachoma kuku hao inalenga kuzuia kuenea kwa homa ya ndege. ''Hakuna haja ya kuathiri sekta yote ya kuku kwa sababu ya vifaranga 5000'', Mashingo alinukuliwa na gazeti hilo akisema. Takriban miezi mitatu iliopita, Tanzania ilichoma vifaranga 6,400 vya kuku wenye thamani ya shilingi 577,000 waliopatikana katika mpaka huohuo , hatua ilioshutumiwa na wanaharakti wa wanyama kutoka mataifa yote mawili. Uamuzi huo pia ulisababisha vita vya kibiashara kati ya mataifa hayo jirani. Chanzo: BBC

Leo ni siku ya malaria duniani

Image
Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya malaria leo, shirika la afya duniani WHO limefahamisha hapo jana kuwa chanjo ya kwanza ya ugonjwa huo itaanza kufanyiwa majaribio nchini Kenya, Malawi na Ghana kuanzia mwaka 2018. Chanjo hiyo ya kiwango kikubwa ilichukua miongo na mamilioni ya Dola kubuniwa. Mratibu wa mpango wa kutekeleza chanjo hiyo Mary Hamel anasema chanjo hiyo kwa sasa imeshavuka ngazi ya kufanyiwa uchunguzi katika maabara na shirika la kudhibiti dawa la Ulaya limeisifu chanjo hiyo. Chanjo hiyo iitwayo RTS,S ni kwaajili ya kuwakinga watoto wadogo dhidi ya aina mbaya ya malaria inayosababishwa na mbu aitwae Plasmodium falciparum. Itafanyiwa majaribio katika maeneo yatakayochaguliwa na nchi hizo tatu na maeneo hayo yanatakiwa kuwa na visa vingi vya maradhi ya malaria na pia kampeni za kupambana na ugonjwa huo. Kulingana na Hamel, chanjo hiyo itatolewa kwa jumla ya watoto 360,000 walio kati ya umri wa miezi mitano na kumi na saba ili kubainisha iwapo dalili za kinga z...

Polepole: Nape alikengeuka

Image
Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekitaka chama hicho kumwajibisha Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kwa kauli yake kuwa alikitoa chama hicho shimoni. Nape, ambaye alikuwa akishikilia nafasi ya Polepole kabla ya Uchaguzi Mkuu, alisema maneno hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Machi 23, siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri. Nape aliyetishiwa bastola kabla ya mkutano huo, alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. “Wamesahau wakati mimi nalala porini, wenyewe walikuwa wanakunywa bia baa.  Nimekuwa mzalendo kwa nchi yangu, nimekuwa muungwana kwa chama changu na ninaapa kuwa muungwana kwa nchi yangu, hilo hakuna atakayelibadilisha. Lakini mimi nimekuwa mzalendo kwa CCM ambayo nimeikuta kwenye shimo inakwenda,” alisema Nape. Lakini Polepole, ambaye jana alitembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayozalisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, ...

Nyambizi ya jeshi la Marekani imewasili katika pwani ya Korea Kusini

Image
Nyambizi ya jeshi la Marekani  Nyambizi ya jeshi la Marekani imewasili katika pwani ya Korea Kusini huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu uwezekano wa Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la kombora au silaha za nyuklia. Meli hiyo kwa jina USS Michigan, ambayo ina uwezo wa kushambulia kwa makombora, inatarajiwa kujiunga na kundi jingine la meli za kivita zinazoelekea eneo hilo, zikiongozwa na meli kubwa ya kubeba ndege ya Carl Vinson. Korea Kaskazini inaadhimisha miaka 85 tangu kuanzishwa kwa jeshi lake Jumanne. Miaka ya nyuma, imekuwa ikiadhimisha siku hiyo kwa kuzindua makombora na silaha nyingine. ---Chanzo BBC

Viwavi wanavyotishia kilimo cha mahindi Kenya

Image
Viwavi vikishambulia mazao Kenya na Rwanda ni mataifa ambayo hivi karibuni yamevamiwa na viwavi ambao tayari vimeharibu mimea ya mahindi Kusini na Mashariki mwa Afrika. Viwavi hao wametatiza wakulima sana kwa sababu kemikali zinazotumiwa kuwaua haziwaathiri viwavi hao. Wakulima Magharibi mwa Kenya wana wasiwasi mwingi kwa sababu wadudu hao wanaendelea kusambaa kwa kasi.

Mwizi sugu wa simu Marekani anaswa kwa kutumia App

Image
  Simu zaidi ya 100 zilizokuwa zimeibiwa zilipatikana Mshukiwa wa wizi ambaye inaaminika alikuwa ameiba zaidi ya simu 100 aina ya iPhones amekamatwa nchini Marekani. Mwizi huyo alikamatwa baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu zao kutumia programu tumishi ya Find My iPhone kufuatilia simu zao. Simu hizo zilikuwa zimeibiwa katika tamasha la muziki la Coachella katika jimbo la California, polisi wamesema. App hiyo huonesha ilipo simu ya mtu, na baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu zao kupiga ripoti kwa polisi, maafisa walifuatilia kwa kutumia app hiyo hadi wakamnasa mshukiwa. Walipata zaidi ya simu 100 zikiwa kwenye mfuko wa mshukiwa huyo wa wizi.   Simu mpya ya iPhone isiyotumia headphone   Udhaifu mkubwa wagunduliwa kwenye simu za iPhone Baadhi ya simu zilirejeshewa wenyewe papo hapo. Nyingine zimekabidhiwa kwa wasimamizi wanaokusanya mali na bidhaa zilizopotea wakati wa tamasha hilo. Polisi walikuwa tayari wametumwa kwa wingi katika tamasha...

Chama cha AfD chapata viongozi wapya

Image
Alexander Gauland na Alice Weidel ndio watakaoongoza juhudi za chama cha AfD kuingia katika bunge la Ujerumani katika uchaguzi mkuu wa Septemba 24. Alexander Gauland na Alice Weidel Hii ni baada ya wanachama wa chama hicho kuwachagua Jumapili, katika mkutano mkuu uliofanyika mjini Cologne. Gauland alikuwa mwanachama wa kitambo wa chama cha kihafidhina cha Kansela Angela Merkel na anajulikana kwa matamshi yake makali. Idadi kubwa ya wanachama wa AfD waliwaunga mkono Gauland mwenye umri wa miaka 76 na Weidel aliye na miaka 38 ambaye ni mchumi aliyewahi kufanya kazi benki. Kuchaguliwa kwao kulifuatia tangazo lililowashangaza wengi la kiongozi mwenza wa chama hicho Frauke Petry, ambaye ni sura ya chama hicho, kwamba, hataongoza kampeni za chama hicho jambo ambalo huenda likawapa fursa ya ushindi vyama vyengine kama kile cha kihafidhina cha Kansela Angela Merkel. Gauland ni mmoja wa wanachama walio na ushawishi mkubwa katika chama hicho na ni mmoja wa wapinzani wakuu wa Petry...