VIFARANGA 5000 VYACHOMWA TANZANIA

Tanzania kwa mara nyengine tena imechoma vifaranga 5,000 vya kuku vinavyodaiwa kuingizwa nchini humo kupitia mpaka wa Kaskazini wa Namanga kutoka Kenya.
Tanzania imesema kuwa hatua ya kuwachoma kuku hao inalenga kuzuia kuenea kwa homa ya ndege.
Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya, katibu katika wizara ya mifugo nchini Tanzania Maria Mashingo, amesema kuwa mfanyibiashara aliyeingiza vifaranga hao nchini Tanzania hakuwa na vibali vinavyohitajika .

Tanzania imesema kuwa hatua ya kuwachoma kuku hao inalenga kuzuia kuenea kwa homa ya ndege.

''Hakuna haja ya kuathiri sekta yote ya kuku kwa sababu ya vifaranga 5000'', Mashingo alinukuliwa na gazeti hilo akisema.

Takriban miezi mitatu iliopita, Tanzania ilichoma vifaranga 6,400 vya kuku wenye thamani ya shilingi 577,000 waliopatikana katika mpaka huohuo , hatua ilioshutumiwa na wanaharakti wa wanyama kutoka mataifa yote mawili.

Uamuzi huo pia ulisababisha vita vya kibiashara kati ya mataifa hayo jirani.

Chanzo: BBC

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB