Mwizi sugu wa simu Marekani anaswa kwa kutumia App


 Image result for iphone image


Simu zaidi ya 100 zilizokuwa
zimeibiwa zilipatikana
Mshukiwa wa wizi ambaye inaaminika alikuwa ameiba zaidi ya simu 100 aina ya
iPhones amekamatwa nchini Marekani.

Mwizi huyo alikamatwa baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu zao kutumia
programu tumishi ya Find My iPhone kufuatilia simu zao.

Simu hizo zilikuwa zimeibiwa katika tamasha la muziki la Coachella katika jimbo
la California, polisi wamesema.


App hiyo huonesha ilipo simu ya mtu, na baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu
zao kupiga ripoti kwa polisi, maafisa walifuatilia kwa kutumia app hiyo hadi
wakamnasa mshukiwa.

Walipata zaidi ya simu 100 zikiwa kwenye mfuko wa mshukiwa huyo wa wizi.
  Simu mpya ya iPhone isiyotumia headphone
  Udhaifu mkubwa wagunduliwa kwenye simu za iPhone

Baadhi ya simu zilirejeshewa wenyewe papo hapo.
Nyingine zimekabidhiwa kwa wasimamizi wanaokusanya mali na bidhaa zilizopotea
wakati wa tamasha hilo.

Polisi walikuwa tayari wametumwa kwa wingi katika tamasha hilo baada ya visa vya
wizi wa simu kuongezeka, anasema afisa wa polisi Dan Marshall, akinukuliwa na
mtandao wa Gizmodo.

Lakini wenye simu ndio waliosaidia kunaswa kwa mshukiwa.

Wanaohudhuria tamasha hilo wameshauriwa:
  Kutoweka vitu vyao vya thamani katika mifuko yao ya nyuma
  Kuhakikisha vitu vyao vya thamani hawaviweki pamoja
  Kubeba pochi bandia ili kuwahadaa wachopozi

---Chanzo BBC

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB