Polepole: Nape alikengeuka


Image result for hamphrey polepole

Humphrey Polepole

Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekitaka
chama hicho kumwajibisha Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kwa kauli yake kuwa
alikitoa chama hicho shimoni.

Nape, ambaye alikuwa akishikilia nafasi ya Polepole kabla ya Uchaguzi Mkuu,
alisema maneno hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Machi 23, siku
moja baada ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.


Nape aliyetishiwa bastola kabla ya mkutano huo, alikuwa Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo.


“Wamesahau wakati mimi nalala porini, wenyewe walikuwa wanakunywa bia baa. 
Nimekuwa mzalendo kwa nchi yangu, nimekuwa muungwana kwa chama changu na ninaapa
kuwa muungwana kwa nchi yangu, hilo hakuna atakayelibadilisha. Lakini mimi
nimekuwa mzalendo kwa CCM ambayo nimeikuta kwenye shimo inakwenda,” alisema
Nape.


Lakini Polepole, ambaye jana alitembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi
Communications Limited (MCL) inayozalisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na
Mwanaspoti, alisema kama Nape alitoa kauli hiyo, alikuwa amekengeuka.


“Amekitoa Chama cha Mapinduzi shimoni? Kwamba, wakati anakitoa chama shimoni
wengine walikuwa wanafanya nini?” alihoji  Polepole.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB