Posts

Dr. Slaa Receives A State Reception In Alabama Capitol

Image
Katibu mkuu wa Chadema Dr. Willibrod Slaa katika ziara yake nchini Marekani iliyoandaliwa na umoja wa vyuo vikubwa nchini humo ya kujifunza mambo mbali mbali, imemfikisha leo katika jimbo la Alabama na kupokelewa na wakuu wa jimbo hilo akiwemo Gavana pamoja na Waziri wa biashara. Alabama ni moja ya majimbo yaliyokuwa nyuma sana kiuchumi na kimaendeleo siku za nyuma. Uchumi wake ulitegemea kilimo kwa 90%. Miaka 25 iliyopita, viongozi wake walibuni mikakatati ya kulibadilisha. Leo, Jimbo la Alabama ndio moja ya majimbo yenye viwanda vikubwa vya magari kama Honda, Mercedes Benz, Airbus, Hyundai, Raytheon, Space station, Wallgreens na mengineyo Uchumi wake unakua kwa kasi kubwa. Kupitia kauli mbiu yake ya  “Vision Tanzania”  Dr. Slaa alipata kukutana na viongozi wa jimbo hilo ili aweze kujifunza mbinu ambayo ataweza kuwarudishia watanzania ili nao waondokane na umasikini. Licha ya yote, Gavana wa jimbo hilo pamoja na mawaziri wake, wako tayari kushirikiana na Tanzania kwe...

Redd’s Miss Tanzania 2013 Hapiness Watimanywa atembelea TBL

Image
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Robin Goestzche akimpongeza Redd’s Miss Tanzania 2013,Hapiness Watimanywa wakati alipotembelea TBL jijini Dar es Salaam leo ili kutoa Shukrani zake kwa Kampuni hiyo ambayo ndio mdhamini Mkuu wa Shindano la Redd’s Miss Tanzania.Kushoto ni Mkugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kushila Thomas. Mkugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kushila Thomas akizungumza jambo na Mrembo wa Redd’s Miss Tanzania 2013,Hapiness Watimanywa.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Robin Goestzche. Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Buttala akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari kwenye tafrija fupi ya kumtambulisha Redd’s Miss Tanzania kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Robin Goestzche. Redd’s Miss Tanzania 2013,Hapiness Watimanywa katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi mkuu wa TBL,Robin Goestzche na kushoto ni Mkugenzi wa masoko wa TBL,Kushila ...

RAIS JAKAYA KIKWETE AREJEA NCHINI AKITOKEA MAREKANI NA CANADA

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2013 wakitokea Marekani katika ziara ya kikazi. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda huku Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali akiangalia wakati alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2013 akitokea Marekani katika ziara ya kikazi. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasini wakati alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2013 akitokea Marekani katika ziara ya kikazi. Wanaofuatia ni Mbunge wa Nkenge Mhe. Asumpta Mshama na Mbunge wa Wawi Mhe Hamad Rashid Mohamed. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakilakiwa na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius...

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI KATIKA KIJIJI CHA GYKRUM,ARUSHA

Image
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA), Bi. Ruth Koya akisoma hotuba fupi mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda na Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge. Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akifungua rasmi jiwe la msingi katika mradi wa maji wa kijiji cha Gykrum, Karatu Mjini, mkoani Arusha. Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akipata maelekezo kutoka Kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA), Bi. Ruth Koya pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge. Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge, katikati ni Mama Tunu Pinda. Picha zote na Michuzi Blog

MKUTANO WA DR SLAA WASHINGTON DC WAFANA

Image
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilboard Slaa Jumapili Sept 22, 2013 aliongea na Watanzania wa DMV na vitongoji vyake kuhusu mstakabali mzima wa Tanzania, kisiasa, kiuchumi na huku akigusia mali asili na utalii, kusafirishwa kwa wanyama nje ya nchi kinyemela.  Mwenyekiti wa CHADEMA DMV, Bwn. Kalley Pandukizi akizungumuza na kueleza historia ya tawi la CHADEMA DMV lilivyoanzishwa kabla ya kumkaribisha katibu wa tawi DMV, Bwn. Liberatus Mwang'ombe.  Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilboard Slaa katika picha ya pamoja na Katibu wa CHADEMA DMV Bwn. Liberatus Mwang'ombe. Bi. Josephine Mshumbuzi akiongea na wanaDMV kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilboard Slaa. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Leticia Nyerere. Mama Leticia Nyerere akipeana Mkono na Mchungaji Materu katika Mkutano wa Chadema DMV uliohutubiwa na Dr Slaa Pichani ni baadhi ya Wakazi wa Washington DC (DMV) Waliojitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa. ...

ZIARA YA MHE. HARRISON MWAKYEMBE NCHINI MAREKANI

Image
Mhe. Harrison Mwakyembe alipotembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Tanzania House, Washington DC. Katikati ni Mhe. Waziri Harrison Mwakyembe akiwa na ujumbe wake akiwa na baadhi ya maofisa wa Ubalozi huo Bw. Paul Mwafongo (wa tatu Kushoto) na Bw.Suleiman Saleh (wa tatu kulia). Mhe. Harrison Mwakyembe(Mb.)Waziri wa Uchukuzi akipokewa na mwenyeji wake Bw.Robert Shumake,Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Michigan mara baada ya kuwasili hotelini alikofikia. Mhe.Waziri Mwakyembe katika picha ya pamoja na Bw. Shumake na Bw. Suleiman Saleh,Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ,Washington DC. Juu na chini ni Mhe. Mwakyembe katika taswira mbali mbali na Bw. Joelson, Mmiliki wa kituo cha kufundisha Urubani cha DCT katika ziara yake kituoni hapo ambapo alionyeshwa ndege za aina mbali mbali pamoja na kupata historia ya kituo hicho. Mhe. Harrison Mwakyembe (katikati) na Ujumbe wake Bw. Peter Lupatu , Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri,Wizara ya Uchukuzi, B...

Rais Dkt. Kikwete afungua ubalozi wa Heshima San Francisco

Image
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi ofisi ya ubalozi wa heshima(Honorary Consulate) wa Tanzania jijini San Francisco nchini Marekani leo jioni.Kulia ni Balozi wa heshima wa Tanzania jijini San Francisco Mh.Ahmed Issa na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula na wapili kushoto ni Mke wa Balozi Mama Sherry Julin Issa.   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima wa Tanzania jijini San FranciscoMh.Ahmed Issa,(wapili kushoto) muda mfupi baada ya kufungua ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini San Francisco nchini Marekani leo jioni.Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula na kulia ni mke wa balozi Ahmed Mama Sherry julin Issa.   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio jijini San Francisco Marekani muda mfupi baadaya kufungua ubalozi wa heshima wa Tanzania na kuzungumza nao leo jioni.   Rais Dkt.Jakaya MrishoKikwete akizungumza...