Rais Magufuli alaani mauaji ya askari wanane

Rais John Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari Polisi wanane waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha jana jioni katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu leo inasema askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na wameshambuliwa kwa kupigwa risasi wakiwa wanasafiri kwa gari katika barabara ya Dar es Salaam – Lindi.

Popular posts from this blog

TASWIRA: UZINDUZI RASMI WA KAMPENI ZA CHADEMA KWA UDIWANI WA KATA NNE ZA ARUSHA

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI KATIKA KIJIJI CHA GYKRUM,ARUSHA