Kampuni kubwa ya mawasiliano nchini Kenya Safaricom imekumbwa na matatizo ya kiufundi ambayo yameathiri huduma zake za simu

 M-Pesa, Nairobi

Kampuni kubwa ya mawasiliano nchini Kenya Safaricom imekumbwa na matatizo ya
kiufundi ambayo yameathiri huduma zake za simu.

Safaricom imesema hitilafu hiyo imeathiri huduma zake kote nchini humo.

"Tunakabiliwa na tatizo la kuunganisha simu, data na huduma ya M-Pesa. Tatizo
hili kwa sasa linaangaziwa. Samahani kwa usumbufu," kampuni hiyo imeambiwa
wateja kupitia Twitter.


Jina la kampuni hiyo limeanza kuvuma katika mitandao ya kijamii, wateja wakitaka
kujua nini sababu yao kushindwa kupiga simu na kupokea au kutuma pesa.

Kampuni hiyo imeesema kiini cha matatizo hayo ni hitilafu katika hifadhi data
yake ya GSM, teknolojia inayofanikisha mawasiliano ya simu za rununu duniani.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya, asilimia 71.2 ya watu wanaotumia
simu za rununu Kenya hutumia mtandao wa Safaricom.

Kampuni hiyo ina jumla ya wateja 27.2 milioni wa simu za rununu.
Haki miliki ya picha TWITTER Image caption Majibu ya Safaricom kwa wateja
waliokuwa wakilalamikia kampuni hiyo kwenye Twitter

---Chanzo BBC

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB