Jaji Mutungi aibuka kuhusu vurugu za CUF

Image result for jaji mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi

Dar es Salaam. Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi ameibuka na
kulaani vurugu  zilizotokea juzi katika hoteli ya Vina, Mabibo hapa Dar es
salaam, zinazosemekana kuhusisha wanachama wa CUF.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo mchana Jaji Mutungi amesema, "Ni
ukweli usiopingika kuwa, suala la mgogoro wa uongozi katika chama cha CUF lipo
mahakamani, lakini nikiwa msimamizi wa Sheria ya Vyama vya Siasa na kutambuliwa
na jamii kuwa ni mlezi wa vyama vya siasa; nimelazimika kuwasihi wadau wa siasa
hususani wanachama wa chama cha CUF, kutambua kwamba, kuwapo kwa shauri
mahakamani siyo fursa ya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani, kwani jambo hili
ni uvunjifu wa sheria na linaleta sura mbaya kwa jamii,"

"Ninalaani vurugu hizo, ambazo zilionekana kuvunja amani na utulivu na watu
kuumizwa, tofauti na tunu zetu za Taifa za amani na utulivu. Pia, nawaasa
wanachama wa CUF pamoja na tofauti walizonazo, madhali masuala haya yapo
mahakamani hebu tuheshimu utawala wa sheria."

"Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na hata Jeshi la Polisi lipo kushughulikia
malalamiko yoyote yanayohusu uendeshaji na shughuli za chama chochote cha siasa.
Hivyo, hakuna haja ya wanachama wa chama cha CUF kukiuka taratibu za kuendesha
chama hicho au kujichukulia sheria mkononi."

---Chanzo Mwananchi

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB