‘Chopa’ iliyotumiwa na Lema ikitua viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro muda mfupi kabla ya kuanza mkutano. Chopa hiyo ilizunguka anga la Jiji la Arusha kwa madoido ya aina yake, hususani katika Kata nne za Themi, Kimandolu, Elerai na Kaloleni, halikadhalika eneo la mkutano, huku ikimwaga vipeperushi vya kunadi kampeni za Chadema na wagombea wake. Blog hii ilishuhudia wananchi wakigombea vipeperushi hivyo vikitua chini. Sehemu ya umati wa wananchi wa Jijini Arusha waliojitokeza jana katika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro kuhudhuria Mkutano Mkubwa wa Chadema wa Uzinduzi wa Kampeni za kuwania Udiwani kwa Kata nne zilizoachwa wazi na madiwani waliovuliwa uanchama na Chadema zaidi ya miaka miwili iliyopita. Mbunge wa Arusha Mjini na Mjumbe wa kamati Kuu Chadema, Mh Godbless Lema akihutubia umati wa wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo. Mwenyekiti wa Chadema Wilaya, ambae pia ni Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Arusha na Diwani wa Kata ya Levolosi, Mh Ephata Nanyaro...
Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akikata Utepe kuashiria Ufunguzi wa Skuli ya Secondary huko Donge Muanda Kaskazini Unguja. Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akikunjuwa Kitambaa kuashiria Ufunguzi wa Skuli ya Secondary huko Donge Muanda Kaskazini Unguja. Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akikagua baadhi ya madarasa ya skuli ya Secondary ya Donge Muanda ilioko huko Kaskazini Unguja. Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akipanda Mti katika Uwanja wa Skuli mara baada ya kufungua skuli hio ya Secondary huko Donge Muanda Kaskazini Unguja. Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akitoa hotuba yake ya kufungua skuli ya Donge Muanda ilioko huko Kaskazini Unguja ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi. Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Shadya Karume akitia saini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuhudhuria Ufunguzi wa Skuli ya Secondary huko Donge Muanda Kaskazini Unguja. Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Aman...