MAMA SALMA KIKWETE ACHANGISHA SHILINGI MILIONI 142.5 HARAMBEE YA MONTAGECHARITY BALL

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage (iliyoandaa hafla hiyo),Teddy Mapunda akimpa zawadi ya heshima Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete mara baada ya kuifanikisha vyema tafrija hiyo maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage (iliyoandaa hafla hiyo),Teddy Mapunda pichani kushoto akizungumza machache mbele ya meza kuu kabla ya kumpa zawadi ya heshima Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete mara baada ya kuifanikisha vyema tafrija hiyo maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana.Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal.


Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BOT),Bwa.Benno Ndulu cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia Milioni Kumi kwenye hafla ya kukusanya kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali,
Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal pichani kulia akizungumza machache,ambaye pia alichangia kiasi cha shilingi Milioni mbili katika hafla hiyo.
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa pongezi na kumkabidhi cheti cha heshima Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal kwa kuchangia kwake.
Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti cha heshim mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Powerbreakfast kutoka Clouds FM,Said Bonge a.k.a Bonge Barabarani ambaye pia alichangia kiasi cha shilingi laki tisa.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi mmoja wa Wakilishi wa Kampuni ya ndege ya Flight Link cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia kiasi cha fedha kwenye hafla hiyo.