WAZIRI MKUU AMZAWADIA PIKIPIKI BIBI SHAMBA


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitaka maelezo zaidi kuhusu aina ya mbegu ya mahindi iliyotumika kutoka kwa Bi. Grace Hokororo ambaye ni Bibishamba wa kata ya Itenka wakati alipokuwa akikagua shamba darasa analolisimamia kwenye kijiji cha Itenka wilayani Mlele, Katavi, jana jioni (Januari 6, 2013). Alifurahia kazi yake na kuahidi kumpatia pikipiki imsaidie kutembelea vijijiji vingine vinne anavyovisimamia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Bibishamba wa kata ya Itenka, Bi. Grace Hokororo akipokea zawadi ya sh. 305,000/-  kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambazo zilichangwa papo hapo na watu alioandamana nao ili kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya kwenye shamba darasa. Wa pili kulia ni Bw. Joseph Laurent anayesimamiwa na bibishamba huyo ambaye shamba lake lilikaguliwa na Waziri Mkuu katika kijiji cha Itenka jana jioni  (Januari 6, 2013) wilayani Mlele, Katavi. Pia aliahidiwa kupatiwa pikipiki ili imsaidie kutembelea vijijiji vingine vinne anavyovisimamia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB