SEKRETARIETI YA CCM YAENDA KIGOMA KWA TRENI


Wajumbe wa sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiongozwa na Katibu Mkuu, Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana leo wameanza safari ya kuelekea Mkoani Kigoma kwa njia ya reli ya Kati.

Wajumbe hao wanne, Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katibu wa Organization, Dk. Mohamed Seif Khatib, Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro wameanza safari hiyo mchana wa saa 8:30 ikiwa ni moja ya Harakati za kuiunga mkono serikali kufufua usafiri huo muhimu kwa watu wa Kanda ya Magharibu kwa Mikoa ya Shinyanga, Tabora na Kigoma.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kupanda treni hiyo, Kinana alisema ufufuaji wa reli ya Kati ni moja ya Ilani za Chama cha Mapinduzi katika utekelezaji wa Maisha Bora kwa Kila Mtanzania. Pia wamelipongeza Shirika la Reli nchini kwa ufanisi wa haraka kwa kufufua reli hiyo.

Nape akiagana na wana CCM mkoa wa Dar es Salaam

Abiria wakiwa katiaka Behjewa la 3rd Class
Abiria akipunga upepo
Katibu Mkuu wa CCM alipokuwa akielekea kuapanda Treni
Wana CCM Dar es Salaam walipoisindikiza Secretarieti
 Katibu Mkuu wa CCM akisoma kitabu ndani ya treni wakati wa safari
Nape akiwa chumbani kwakwe
Dk. Khatibu akizungumza na Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam, Madabida
         Wana Dar es Salaam wakiimba na kucheza

Popular posts from this blog

TASWIRA: UZINDUZI RASMI WA KAMPENI ZA CHADEMA KWA UDIWANI WA KATA NNE ZA ARUSHA

RAIS KIKWETE ASAIDIA KUENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA WODI YA DHARURA YA WATOTO NA VIFAA VYAKE HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI