Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Orly, Ufaransa, baada ya kumaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tano nchini humo leo Januari 23, 2013.
‘Chopa’ iliyotumiwa na Lema ikitua viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro muda mfupi kabla ya kuanza mkutano. Chopa hiyo ilizunguka anga la Jiji la Arusha kwa madoido ya aina yake, hususani katika Kata nne za Themi, Kimandolu, Elerai na Kaloleni, halikadhalika eneo la mkutano, huku ikimwaga vipeperushi vya kunadi kampeni za Chadema na wagombea wake. Blog hii ilishuhudia wananchi wakigombea vipeperushi hivyo vikitua chini. Sehemu ya umati wa wananchi wa Jijini Arusha waliojitokeza jana katika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro kuhudhuria Mkutano Mkubwa wa Chadema wa Uzinduzi wa Kampeni za kuwania Udiwani kwa Kata nne zilizoachwa wazi na madiwani waliovuliwa uanchama na Chadema zaidi ya miaka miwili iliyopita. Mbunge wa Arusha Mjini na Mjumbe wa kamati Kuu Chadema, Mh Godbless Lema akihutubia umati wa wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo. Mwenyekiti wa Chadema Wilaya, ambae pia ni Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Arusha na Diwani wa Kata ya Levolosi, Mh Ephata Nanyaro...
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA), Bi. Ruth Koya akisoma hotuba fupi mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda na Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge. Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akifungua rasmi jiwe la msingi katika mradi wa maji wa kijiji cha Gykrum, Karatu Mjini, mkoani Arusha. Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akipata maelekezo kutoka Kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA), Bi. Ruth Koya pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge. Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge, katikati ni Mama Tunu Pinda. Picha zote na Michuzi Blog