IKULU:Rais Jakaya Kikwete Ampokea Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Benin,Dkt. Boni Yayi

Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akimkaribisha mgeni wake Mheshimiwa Dkt.Boni Yayi wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu julius Nyerere usiku wa Jana Usiku
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Dkt.Boni Yayi wakifurahia jambo katika hoteli ya Kilimanjaro Jana usiku.


Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Benin, Mheshimiwa Dkt. Boni Yayi amewasili nchini usiku wa jana, Jumanne, Januari 15, 2013, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, Rais Boni Yayi amepokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mara ndege yake ilipotua kiasi cha saa tano unusu usiku.Leo asubuhi, viongozi hao wawili watafanya mazungumzo rasmi kabla ya Rais Boni Yayi kuondoka nchini kuendelea na ziara yake Barani Afrika.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB