MWAKYEMBE ADAKA WATANO WAKITAKA KUVUSHA MALORI 26 KINYEMELA BANDARINI



Waziri wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe akizungumza na waadishi wa habari 

Bandarini jijini Dar es salaam leo jioni wakati akitoa taarifa ya 
kukamatwa kwa watumishi wa Bandari wanaodaiwa kutaka kutoa  malori 26 
kinyemela  bandarini, watu watano wamekamatwa katika sakata hilo.




Dk.Harrison Mwakyembe akiongea na maafisa mbalimbali wa Polisi na Bandari 

baada ya kukagua magari hayo yaliyotaka kutolewa kinyemela bandarini 
hapo.




Dk.Mwakyembe akikagua Malori yanayodaiwa  kutaka kutolewa kinyemela na 

kampuni ya Dhandho, Malori matano kati ya 26 yalipewa baraka na Mamlaka 
ya Mapato Tanzania (TRA) yatolewe.




Mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Andrew Masaga (kulia) 

anayedaiwa kuhusika kula njama ya kutoa malori hayo  akijitetea mbele ya
Waziri (hayupo pichani) katika sakata hilo leo jinoni. Kushoto  ni Mkuu
wa Polisi Bandarini Afande FM MisilimuOfisa Utawala wa kampuni ya Dhandho Antipasi Otieno (kulia) akitoa maelezo mbele ya waziri Dk. Harrison Mwakyembe




 
Mtumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Gladness Mangelele akitoa maelezo

mbele ya Waziri Dk. Mwakyembe baada ya kuhusishwa katika sakata hilo 
ambapo alidai alikuwa hajui chochote kwani alikuwa  akitekeleza majukumu
yake ya kawaida katika idara yake.




Marystella Minja akitoa maelezo yake mbele ya Waziri Dk Harrison Mwakyembe baada ya kutuhumiwa katika sakata hilo.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB