RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI YALIYOFANYIKA KITAIFA MKOANI LINDI JANA

Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu Mjini Lindi, huku wadau mbalimbali wa masuala ya mapambano ya ukimwi wakishiriki kwa kufanya maonyesho na kutoa elimu na maelezo mbalimbali yanayohusu mapambano ya ukimwi, Rais Pia ameshuhudia utiwaji saini wa msaada wa Dola za Kimarekani Milioni 308 kutoka mfuko wa Global Fund uliosainiwa kati ya Katibu katibu wa Ofisi ya rais Paniel Lyimo na Ramadhan Kijahkati Kabu Mkuu Wizara ya Fedha huku Mfuko wa Global Fund ukiwakilishwa na Christoph Benn Mkurugenzi wa mfuko huo. 

Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi tuzo Mke wake Mama Salma Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA kwa kutambua mchango wa taasisi hiyo katika mapambano ya Ukimwi wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kitaifa iliadhimishwa  mkoani Lindi kwenye uwanja wa Ilulu na kushirikisha wadau mbalimbali wanaopambana na janga la ugonjwa wa ukimwi, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila.


Rais jakaya Kikwete akimkabidhi tuzo Meneja wa PSI Mtwara na Lindi  kwa kutambua mchango wa taasisi hiyo katika mapambano ya ukimwi wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika jana mjini Lindi, kushoto ni Mkurugenzi wa Tume ya kudhibiti Ukimwi TACAIDS Dr. Fatma Mrisho.

Rais Jakaya Kikwete akisalimia wafanyakazi wa kampuni ya simu ya TTCL wakati akitembelea mabanda katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiinua juu kitabu kuzindua rasmi mpango wa Kutokomeza maambukizi ya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto(Prevention From mother To Child Trsnsmission(PMTCT) wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Ilulu mjini Lindi jana. Wengine katika picha ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete(kulia),Waziri wa Afya Dkt.Hussein Mwinyi(wanne kushoto), Mkurugenzi wa Global fund Dkt.Christopher Ben(kushoto) na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bwana Ludovic Mwananzila(picha na Freddy Maro)

Popular posts from this blog

TASWIRA: UZINDUZI RASMI WA KAMPENI ZA CHADEMA KWA UDIWANI WA KATA NNE ZA ARUSHA

RAIS KIKWETE ASAIDIA KUENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA WODI YA DHARURA YA WATOTO NA VIFAA VYAKE HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI