Makamu wa rais Dkt. Bilal azindua jengo jipya la ofisi za kampuni ya usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi (DHL).



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa DHL Blaise D’sauza, wakati alipokuwa akitembelea katika jengo jipya la Kampuni ya usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi (DHL), baada ya kuzindua rasmi jengo hilo lililopo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki. 
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Usimamizi wa Uingizaji wa Mizigo, Buzegi Kulwa (kulia) wakati alipokuwa akitembelea katika jengo jipya la Kampuni ya usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi, (DHL) baada ya kuzindua rasmi jengo hilo. 
  Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi wa huduma kwa Wateja upande wa uingizaji wa mizigo, Ebtisam Bobsaith (kushoto), wakati alipokuwa akitembelea katika jengo jipya la Kampuni ya usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi, (DHL) baada ya kuzindua rasmi jengo hilo.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa DHL, Blaise D’sauza (wa pili kushoto) ni Meneja Usimamizi wa Uingizaji wa Mizigo, Buzegi Kulwa na (wa tatu kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki.


  Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo  wakati akiendelea kutembelea katika jengo hilo jipya la Kampuni ya usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi, (DHL) baada ya kuzindua rasmi jengo hilo.   
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya uzinduzi jengo jipya la Kampuni ya usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi, DHL wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa jengo hilo.
 Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkurugenzi Mkuu wa DHL Blaise D’sauza, wakifunua kitambaa kwa pamoja kuwashiria uzinduzi wa jengo jipya la Kampuni ya Usafirishaji wa Mizigo ndani na nje ya nchi (DHL), wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Uchukuzi Mh.Dkt. Harrison Mwakyembe. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa DHL Blaise D’sauza, mara baada ya uzinduzi wa jengo jipya la Kampuni ya usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi, (DHL) lililopo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki. (Picha na OMR).

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB