Jocelyine Maro Alipoibuka Mshindi Miss East Tanzania


Jocelyne Maro Mii East Africa Tanzania akipunga mkono kwa mashabiki wake mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam akiwashinda warembo wenzake kutoka mataifa mbalimbali ya Ukanda wa Afrika Mashariki na nchi Jirani na Ukanda huo.
Jocelyne Maro Mtanzania wa kwanza kushinda taji hilo toka lililpoanzishwa amejinyakulia zawadi zenye tmamani ya dola za kimarekani 30,000 likiwemo Gari aina ya Toyota Verossa, mara baada ya majaji kumtangaza mrembo huyo ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe huku watu mbalimbali wakimpongeza kwa ushindi wake PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akipiga picha ya pamoja na Miss Uganda Ayisha Nagudi mshindi wa pili katika shindano hilo kushoto na Miss Burundi Ariela Kwizera ambaye alipata nafasi ya tatu katika shindano hilo.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akipiga picha ya pamoja na warembo wenzake alioingia nao kwenye tano bora ya shindano hilo.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akiwa amepigwa na butwaa mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo jana usiku.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akipongezwa na wenzake mara baada ya kushinda katika shindano hilo.

Popular posts from this blog

RAIS KIKWETE AZINDUA MPANGO WA HUDUMA POPOTE WA BENKI YA POSTA TANZANIA TPB